SERIKALI YATAKIWA KULINDA UCHOCHEZI DHIDI YA MGODI WA BARRICK NORTH MARA
Serikali imetakiwa kuulinda kwa nguvu zote mgodi wa Dhahabu wa North Mara kutokana na mashambulizi yasiyo ya haki inayopata kutoka kwa wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu.
Mwenyekiti wa Muungano wa koo 12 za jamii ya wakurya wilayani Tarime, Mzee Mwikwabe Makabe amesema haya hivi karibuni mjini Tarime wakati akielezea mahusiano mazuri yaliyopo sasa kati ya mgodi huo na wananchi wa jamii zinazozunguka mgodi huo.
Alieleza kuwa kwa muda mrefu asasi za kimataifa na baadhi za ndani zimeugeuza mgodi huo kama eneo la mashambulizi kwa manufaa binfasi kwa kwenda kufanya utafiti usio rasmi na baadae kutoa ripoti zinzopotosha haki halisi ilivyo katika jamii hizo na jinsi znavyohusiana na mgodi huo.
“Tunaiomba serikali ichukue hatua kwa hawa watu wanakuja wanazunguzunguka humu bila taarifa za mamlaka wakitoa hapa wanakwenda kuharibu sifa nzuri ya mgodi,” Mwikwabe makabe Mwenyekiti wa Muungano koo12.
Alieleza kuwa mgodi huu nguzo ya maisha ya watu wa maeneo yote yayozunguka mgodi, wanaouhujumu wanatuhujumu sisi, wanataka wananchi wasiendelee kupata maendeleo tunayoyaona sasa, sisi wazee wa mila hatutaruhusu watu waje kutuharibia maendeleo yetu sasa hivi hali ni nzuri na sisi kama wazee tunataka watu wetu, vijana wetu wapate maendeleo na huduma kwa ukaribu”.
Mwezi Juni mwaka huu baadhi ya wanaharakati wamefungua kezi itakayosikilizwa katika Mahakama Kuu ya London.
Mashtaka yaliyofunguliwa na kampuni ya sheria ya Uingereza Leigh Day kwa niaba ya familia za watu wawili wanaodaiwa kuuawa na askari wakati wamevamia mgodi (intruders) dhidi ya Mamlaka kuu ya kimataifa inayosimamia biashara ya dhahabu na fedha duniani kote, London Bullion Martket Association (LBMA) inaweza kusababisha kufungwa kwa mgodi huo.
LBMA ni mamlaka yenye majukumu ya kuweka viwango vya ubora (Good delivery list) kwenye dhahabu zinazouzwa kwenye masoko makubwa duniani ni uhakikisho wa kwamba dhahabu hiyo inachimbwa katika mazingira salama.
Leidh Day wanaishtaki LBMA ili iondoe dhahabu zinazochibwa katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwenye orodha yao ya good delivery kwa madai kwamba zinanachimbwa katika mazingira yanayokiuka haki za binadamu.
Akizungumzia hali hiyo mtalaamu mmoja wa sheria za madini katika moja ya ofisi za madini katika mikoa ya ukanda wa ziwa, alisema kuwa ni LBMA ni kiini cha mfumo wa biashara ya dhahabu dunia, kama ikishindwa kesi hiyo itamaanisha North Mara kusimamisha uzalishaji hali ambayo itaathiri ukuaji wa mchango wa sekta ya madini nchini ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
“Tafsiri yake iko moja kwa moja, kama kama hao wanaharakati wakishinda kesi, ni wazi North Mara hatakuwa na mhala pa kuuza dhahabu, atalazimika kusimamisha uzalishaji na hiyo maana yake ni kukoma kwa ajira, miradi ya CSR na mapato ambayo serikali, halmashauri, vijiji wamekuwa wakiyapata kutokana na uzalishaji wa mgodi huo,” anasema mtaalamu huyo ambaye aliomba kutotajwa jina lake kwa sababu siyo msemaji wa ofisi yake.
Tangu mwaka 2019 hadi sasa Mgodi wa North Mara umechagia katika Uchumi wa Tanzania kiasi cha dola za kimarekani bilioni 4.79 na katika robo ya pili ya mwaka jana 2025 pekee ulichagia Dola Milioni 558. Hii ni mbali na michango mingine kama kufanya manunuzi kutoka soko la ndani yanayofikia dola milioni 83.
Kupitia kanuani ya maudhui ya ndani kamapuni hiyo mwaka 2024 zaidi ya asilimia 83 ya manunuzi iliyofanya yalifanywa na kampuni za kitanzania, pesa iliyolipwa kwa wakandarasi wa kitanzania mwaka huo ni dola milioni 573 sawa na shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni 140.
Hadi kufikia Oktoba mwaka jana 2025 kupitia ubia wa Twiga Minerals Corpotaration ililipa dola bilioni 1.37 kama kodi, mrabaha na ushuru Pamoja na kodi ya mapato ya ya dola milioni 92 mwaka 2024
Hii itamaanisha pia kuwa gawio la asilimia 50 ya faida ambalo serikali inapata kupitia hisa zake kwenye kampuni ya Twiga Minerals zitakosekana, watanzania kwa maelfu walioajiriwa huko watapoteza ajira, makampuni ya kitanzania ambayo kwa sasa yanafaidika na uwepo wa mgodi huo kupitia sheria ya local content watakosa biashara na wafanyakazi wao watakosa ajira.


