Mtazamo wa Viongozi wafanyabiashara juu ya Mazingira ya Uwekezaji Tanzania kwa mwaka 2015 umeonesha Rushwa


feature_041013
umeonesha Rushwa, Viwango vya Kodi na Usimamizi wa kodi, kama mambo yanayosababisha ugumu wa kufanya biashara kwenye mikoa mingi nchini.

Kwa mujibu wa utafiti wa sita uliofanywa Julai – Agosti mwaka jana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania na kuhusisha wamiliki na maafisa watendaji 597 kutoka mashirika, taasisi na kampuni nyingi, za kati na kubwa, umeonesha matatizo ya Umeme, Maji na Barabara yamekithiri mkoani Mbeya, mkoa wa Arusha ukikithiri na Vitendo vya Rushwa huku Viwango na Usimamizi wa Kodi ukiwa kikwazo mkoani Dar es salaam.
Ripoti hiyo iliyofadhiliwa na Mpango wa mazungumzo ya Uwezeshaji Mazingira ya Kibiashara Tanzania ujulikanao kwa kifupi BEST – Dialogue,imeonesha katika serikali iliyopita, Rushwa ilikithiri kwenye sekta nyingi, huku ikiainisha baadhi yake kuwa ni Sekta ya Fedha, Biashara, Ujenzi, Viwanda na Utalii.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani mara baada ya kuzinduliwa kwa Ripoti hiyo yenye Kurasa 25, baadhi ya wadau wa sekta binafsi wamependekeza serikali kubadilisha mfumo wa kodi, ambao wamedai utasaidia kudhibiti Rushwa pamoja na kutanua wigo wa upatikanaji wa mitaji .
Licha ya kwamba Ripoti hiyo imeonesha mawazo ya viongozi wafanyabiashara kwa serikali ya awamu iliyopita, Baadhi ya wadau wa vyama na Taasisi za wafanyabiashara, wameonesha imani kubwa kwa serikali ya awamu ya Tano,  hasa kutokana na utashi wa kisiasa alio nao wa kudhibiti Rushwa na kurejesha nidhamu ya kazi kwa watendaji wa taasisi za umma.
Powered by Blogger.