RC MARA AUNDA TIMU YA WAJUMBE NANE KUFATILIA ILIKO TIMU YA BIASHARA UNITED MARA.

 

Mkuu wa mkoa wa Mara kanali Evans Mtambi ameunda Timu ya wajumbe Nane (8) ya kufatilia na kufanya Tathimini Juu ya Mwenenndo wa Timu ya Biashara United Mara ambayo itaongozwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma ambapo itatakiwa kutoa Mresho kwa kipindi cha mwezi moja baada ya kukamilisha zoezi iliyopewa.

kanali Mtambi ametoa kauli hiyo baada ya Mjumbe  Abdallah Mohamed kutoa hoja kufutaia mkoa wa Mara kutokuwa na timu yoyote ya mpira wa miguu mkoani humo ambapo amesema ujkosefu wa timu katika mkoa wa Mara umepelekea mkoa kudorola katika kichezo hivyo kumuomba mwenyekiti wa kikao hicho kuangalia namna mkoa huo kupata timu.

"kufuatia mwenendo wa timu ya Baishara United Mara kutokueleweka na  kumepelekea sisi kukosa timu kwenye mkoa wetu ndugu mwenyekiti tunakuomba tupate Timu nasisi tumezimis simba na Yanga  kwenye mkoa wetu"Alisema Abdallah Mdau wa Michezo  na katibu wa AC -WAZALENDO Mkoa wa Mara.

aidha baada ya hoja hiyo Mkuu wa mkoa wa Mara akaunda Timu ya watu nane ambayo itaongozwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka,Mwita Waitara,Mgore Miraji Kigera,Gimbana Ntavyo,Abdallah Mahamoud na Dolnard Mwembe.



Powered by Blogger.