AGNESS MARWA AWAKUMBUSHA WALIMU KUONGEZA MBINU ZA UFUNDISHAJI.
Walimu wakuu wa shule za msingi na maafisa Elimu kata katika manispaa ya Musoma mkoani Mara ,wametakiwa kuongeza mbinu za ufundishaji na ushirikiano katika ufundishaji ilikuboresha ufaulu kwa wanafunzi nakuondokana na matokeo mabaya mitihani ya miaka miwili mfulilizo uliyoyapata mkoa wa Mara.
Rai hiyo inatolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa wakati akizungumza na watendaji hao wa idara ya elimu katika ukumb i wa manispaa ya Musoma mkoani Mara ambapo amesema mkoa wa Mara haufanani na matokeo yanayoendelea kuuandama mkoa huo ya kitaifa.
Agness amesema anatarajia kuanzisha pia mashindano ya ondoa zero katika mkoa huo ilikuisaidia serikali katika mapambano ya elimu na kuunga mkono juhudi za Dkt Samia Suluhu Hassan za kuboresha ufaulu nchini.
“Tunaenda kuanzisha mashindano na kutoa motisha
yaondoa zero kwa walimu watakaofanya vizuri katika matokeo ya kitaifa mkoa wetu
unarasilimali nyingi ambazo zinawezesha walimu kufanya vizuri katika matokeo
yao lakini sasa tumekuwa tukifanya vibaya niwakati wakuamka kuondoa zero mara”Aliasema Agness Marwa Mbunge wa Viti Maalum Mara.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wawalimu wakuu katika
manispaa ya Musoma Mkoani Mara Veneranda Biseko alisema motisha hiyo
inasaidia wao kuja na mbinu mpya za kuongeza ufaulu nakufanya vizuri katika
mitihani ya kitaifa.