MILIONI 36 KUMTOA KATIBU WAZAZI KWENYE NYUMBA YA KUPANGA
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Mara Patrick Chandi ameongoza kupatikana na shilingi Milioni 27 –kati
ya milioni 36 zinazohitajika kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya katibu wa Jumuiya
ya Wazazi wilaya ya Butiama mkoani Mara kufutia katibu huyo kuishi katika
nyumba ya kupanga .
Harambee
hiyo ambayo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya wazazi chandi amewataka
viongozi hao kutokutumia fedha hizo kugawana posho na mambo mengine badala yake
ujenzi wa nyumba hiyo uanze mara moja.
Akizungumza
mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Julius Masubo amekiomba chama cha
mapinduzi makao makuu kupitisha upya oparesheni ya kubaini mali za chama kwani
badao ziko nyumba za chama cha mapinduzi mikononi mwa watu nazinawanufaisha wao
badala ya jumuiya.
“Sinyumba pekee vipo hadi viwanja magari yako mikononi mwa watu mfano sisi tunanyumba iko Tarime kule mpakani tulipelekana hadi mahakamani na kesi tukashinda nasisitunatamani tukabidhiwe hiyo nyumba niombe viongozi wetu wa juu wafatilie mali hizi nazipate hatimiliki nazile za jumuiya tukabidhiwe”Alisema Masubo Kambarage.
Aidha chandi amewataka wana mara wanaoishi nje ya mkoa huo kurejea kujenga nyumbani kwao kwani mkoa wa Mara utajengwa na wanamara wenyewe na wasiwatu wengine kutoka nje.