Mfumo ilioundwa na NECTA wa kutunza taarifa za wanafunzi wa shule za msingi

Baraza la mitihani Tanzania – NECTA limefanikiwa kuunda mfumo wa kutunza taarifa za wanafunzi wa shule za msingi hatua ambayo itasaidia katika suala la uandikishaji kwa kutoa namba maalumu ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo.
Akziungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwa niaba ya katibu mtendaji NECTA afisa habari NECTA John Nchimbi alipokuwa akizungmzia mafanikio ya baraza hilo, amesema mfumo huo pia utasaidia katika kurahisisha utaratibu wa unaotumika sasa wa kuhamisha wanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine lakini pia utaweza kuondoa tatizo la wanafunzi hewa na kwa majaribio mfumo huo umeanza kufanya kazi katika mikoa ya Mwanza na Ruvuma huku ukitarajiwa kuanza rasmi januari mwakani katika mikoa yote.
Akizungumzia changamoto zinalikabili baraza hilo Afisa mitihani NECTA Khalfan Kabiki amesema linakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha jambo ambalo linakwamisha utekelezaji wa baadhi ya majukumu pamoja na ufinyu wa sehemu ya kuhifadhia nyaraka.
Powered by Blogger.