CHOMETE AIKUMBUSHA SERIKALI KUPELEKA FEDHA KWENYE MIRADI YA MAJI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Ghati Zephania ameomba Serikali kupeleka Fedha zilizoombwa ili kukamilisha Miradi ya Maji Mkoani Mara na kutumiza lengo la DKT Samia Suluhu Hassan la kumtua mama ndoo kichwani
Chomete etoa kauli hiyo katika Bunge la Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2026-2027 ambapo amesema kucheleweshwa kwa Fedha za miradi hiyo ya maji katika Wilaya na Mkoa wa Mara kunazidi kuwaathiri wananchi katika kupata huduma hiyo muhimu katika jamii, pamoja na kuathiri kabisa shughuli za Kiuchumi na kijamii.
