*MBUNGE VITI MAALUM MARA GHATI CHOMETE ASHIRIKI MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO YA USHIRIKA& UZINDUZI WA KAMPENI YA UADILIFU KATIKA USHIRIKA*



Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Bi.Ghati Chomete akishiriki katika uzinduzi wa kampeni y ya Uadilifu katika ushirika 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete amemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya Ushirika pamoja na Uzinduzi wa Kampeni ya Uadilifu katika Ushirika katika Ukumbi wa PSSSF, Jijini Dodoma.

Mhe.Ghati amesisitiza kuwa Vyama vya Ushirika vinapaswa kuimarisha usimamizi na uwajibikaji kwa wanachama wao kwa uwazi na uadilifu na kuwajengea uwezo mafunzo ya kisasa ya biashara, masoko na usimamizi wa fedha.

Mhe.Ghati aliongeza kuwa hatuwezi kuzungumzia Maendeleo ya ushirika bila kugusa viwanda ambavyo huongeza thamani ya mazao.

Aidha, alisema kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha upatikanaji wa mitaji na mikopo nafuu ili vyama viweze kujiendesha kibiashara.

Powered by Blogger.