TARURA MARA WATUMIA TEKNLOJIA YA MAWE KUJENGA MADARAJA
Meneja Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini Tarura mkoa wa Mara Mhandisi Wiliam Lameck amesema ujenzi wa kutumia teknlojia yamawe katika madaraja imekuwa njia bora na imara lakini imesaidia kuopunguza gharama za ujenzi
Mhandisi lameck ametoa kauli hiyo wakati akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la mawe katika mto tigite linalounganisha vijiji vya Nyarwana na matongo halamshauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara ambapo alisema ujenzi wa madaraja kwa mawe nibora naniimara ukilinganisha na ujenzi wa kutumia nondo pamoja na mawe ambayo imekuwa
Akizungumza meneja wakala ya Barabara Mijini na Vijijini Mkoa wa Mara Mhandisi Wiliam Lameck amesema njia hiyo nibora ambayo inafanya madaraja kudumu kwa takribani miaka 100 lakini pia inasaidiakupunguza gharama za ujenzi.
“Madaraja haya nimazuri nayako imara ambayo yanaeza kukaa miaka 100 na zaidi na ghamayake nirahisi kutokana mawe kupatikana katikaeneo la mradi unaweza kutumia daraja hili zege na vyuma inaweza kuchukua Bilioni 1 na kitu lakini hili la mawe linachukua milioni 300 hai 500 kwahiyo madraja haya nimhimu sana”Alisema Eng Wiliam Lameck Meneja wa Tarura Mkoa wa Mara.
Wananchi wanaoishi maeneo hayo wameishukuru serikali kwa kujenga daraja kwani eneo hilo walikuwa wanalazimika kuvuka katika daraja la miti ambalo lilikuwa likihatarisha maisha yao.
MWISHO