WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA JKT KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (Mb), Tarehe 26 Machi 2026, Bungeni jijini Dodoma amewasilisha kwa kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mambo ya nje, ulinzi na Usalama-NUU , taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi Cha kuanzia julai 2026 hadi Februari 2027.
Kamati hiyo ya NUU inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Nasma Murtaza Giga (Mb) pia ilipokea taarifa ya Wizara ya Ulinzi na JKT na mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Ulinzi ya SUMMA JKT, MZINGA na NYUMBU.
Waziri wa Ulinzi na JKT katika uwasilishaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa bajeti kwa kamati ya NUU aliambatana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Dkt.Faraji Kasidi Mnyepe
.jpeg)
