WAGANGA WA TIBA ASILI WANOLEWA ILI KUWAONGEZEA MAARIFA.

 


Na Mwandishi wetu Mwanza

Waganga wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Mwanza wamepatiwa elimu mahususi yenyekuwajengea uwezo  na maarifa katika utendaji kazi wa utoaji huduma ya tiba kwa wananchi.

Akitoa elimu hiyo  kwa waganga wilaya ya Ilemela  mkoani Mwanza katibu mkuu wa chama cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala Bw Lukas Joseph Mlipu amesema kwamba chama hicho kimejenga misingi mbalimbali ikiwemo ya kuwapa elimu waganga wanaojiunga na chama hicho kwa lengo la kuchechemua taaluma hiyo ambayo imekuwa ikizipitia changamoto nyingi kutokana na sababu tofauti tofauti  ikiwemo ya waganga kuchukuliwa kama watu wasiokuwa na elimu jamba ambalo  siyo sahihi hivyo ili kuiondoa dhana hiyo kwa jamii TAMESOT iliona vyema  kuanzisha    mpango  mahususi  wa kuwasadia  waganga kwa kuwapa  elimu  wanaojiunga na chama hicho.

Bw Mlipu  akiwa darasani amesema ili kuyafanikisha malengo hayo tayari  kwa umahiri mkubwa chama kimechapisha vitabu kadhaa ambavyo ndani yake vipo vya  miongozo kwa viongozi na miongozo ya wanachama sambamba na vitabu vya katiba na kanuni za  TAMESOT.

Kiongozi huyo pia amesema yuko kwenye ziara ya mikoa 10 akiendelea kukutana na waganga  pamoja na wadau likiwemo jeshi la polisi akiendelea kuwahamasisha mambo muhimu likiwemo suala la kupata uongozi imara  kuanzia ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya chini ili kushirikiana na mamlaka za serikali katika kuwaunganisha pamoja  waganga hatimaye waweze kufanya kazi zao kwa uhuru bila kubughudhiwa. 

Amafafanua kuwa tayari ziara yake imeifikia mikoa minne ya Mbeya, Shinyanga, Geita , Mwanza na bado anaendelea na mikoa mingine ukiwemo mkoa wa Mara.

Akiwa mkoa ni Mwanza katibu mkuu Lukas hakusita kukemea watu wanaotumia mwavuli wa tiba asili kinyume na taratibu ili kushiriki ramli chonganishi kwa jamii jambo ambalo amesema halivumiki huku akisisitiza kuwa TAMESOT itaendelea kuwakemea watu wanamna hiyo kwani hawana nia njema na taba asili badala yake wamekuwa ni watu wenye kuichafua kwa matukio maovu ikiwemo ya kuwaibia wananchi na hayuko tayari kumuona mwanachama wa TAMESOT akishiriki ramli chonganishi.

Ametoa wito kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala  kushikamana na kuwa  wamoja katika majukumu ya kuwasadia tiba wananchi tena  kwa ufanisi ambapo amewahimiza kuhakikisha wanashiriki matukio yanayowakusanya kwa pamoja likiwemo tukio linalotarajia kuwakutanisha hivi karbuni waganga na waziri wa afya mkoani Dodoma.

Nao waganga wa mkoa huo wa Mwanza wamepongeza  na kushukuru ujio wa ziara ya katibu mkuu Lukas kutokana na alivyowapatia elimu na maarifa kadha wa kadha nakuwaongezea mwanga zaidi katika majukumu yao ya kutoa tiba hivyo nao hawakusita kuwakemea watu wanaoshiriki ramli chonganishi wakisema kuwa kutokana na madhara ya ramli hiyo watu wanamna hiyo hawanabudi kushughulikiwa ili kuyakomesha matukio yakikatiri ambayo mara kadhaa yamekuwa yakijiri kwa jamii.

Powered by Blogger.