MFANYABIASHARA ALIYEPOTEA ARUSHA AKUTWA AMEFARIKI

 


Ikiwa nisiku kadhaa kuripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mfanyabiashara wa madini, Abdillah Mussa maarufu kama Banjo, mkazi wa Sanawari mkoani Arusha, hatimae mwili wake umekutwa katika eneo la Bereko, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mwili huo ulikutwa ukiwa umeharibika, hali iliyozua maswali mengi kuhusu mazingira ya kifo chake.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mussa Abdillah, familia ilipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa kuna mwili umeokotwa pembezoni mwa barabara katika maeneo ya Bereko, Kondoa. Walipofika eneo hilo, walithibitisha kuwa mwili huo ni wa baba yao, huku ukiwa na majeraha ikiwemo kutobolewa macho na kuvunjwa mkono.

Mussa akizungumza hiyo jana alisema kuwa Februari 12 mwaka huu, baba yake aliondoka nyumbani kuelekea mazoezini katika eneo la jengo la Ngorongoro, lakini baadaye kulikuwa na taarifa kuwa alichukuliwa na watu wasiojulikana.
 
Juhudi za ndugu na jamaa kumtafuta hazikuzaa matunda hadi walipopokea taarifa za kupatikana kwa mwili wake huko Kondoa.

Jeshi la polisi mpaka sasa halijatoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo

Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi zitakujia

Powered by Blogger.