MGORE MIRAJI KUWAPELEKA VETA VIJANA WANAOSHINDA KWENYE VIJIWE VYA POMBE.
Kufutia serikali kuwekeza nguvu kubwa katika kundi la vijana dhidi ya utoaji wa mikopo Mbunge wa jimbo Musoma Mjini Mgore miraji kigera amewataka wazazi katika manispaa ya Musoma kusajili vijana wao wote wanaokaa vijiweni hususani vya pombe ilikuingizwa katika mpango wa mafunzo ya Ufundi stadi Veta.
Kauli hiyo anaitoa baada ya baadhi ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa usomaji utekelezaji wa siku 100 kulalamikia juu ya uwepo wa vijana katika maeneo ya majita road kujiingiza katika mvitendo vya ulevi na makundi ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wawananchi.
Mgore miraji baada ya malalamiko hayo anawataka wananchi hususani wazazi kuhakikisha wanawashirikisha vijana wao katika mikopo ya serikali lakini pia kutumia ofsi za serikali kupata uelewa juu ya mikopo inayotolewa na serikali ilivijana hao kuingizwa katika mpango nakuondoakana na tabia za unywaji wa pombe hovyo.
“Niwaombe wazazi tushirikianeni kuwabaini vijana ilikuwaondoa kwenye makundi hayo tuko tayari kuwapeleka veta nakukikisha wanaachana na vitendo hivyo tunahitaji kuijenga musoma iliyobora nayenye kuhakikisha kila mtu ananufaika na uvuchumi wa Taifa hili”Alisema Mgore Miraji Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Musoma Juma chikoka alisema serikali imekuwa ikitoa fedha kupitia makundi ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu hivyo kamwe hawapaswi kuacha kuchangamkia fursa hiyo.

.jpeg)
