AGNESS MARWA APELEKA TABASAMU KWA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MANISPAA KATIKA MITIHANI YA KITAIFA


 

 

Shule ambazo zimefanya Vizuri katika mitihani ya Kitaifa  Manispaa ya Musoma Mkoani Mara zimetambuliwa na  kupewa zawadi mbalimbali ikiwa ni motisha  kuhakikisha walimu hao  wataendelea kufanya vizuri katika kampeni ya kutokomeza zero katika matokeo ya Kitaifa.

Kampeni hiyo ya kupambana dhidi ya kutokomeza Zero katika Manispaa ya Musoma imeanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma  na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa ameanza kuunga juhudi hiyo kupitia FOUNDATION YA AGNESS TOKOMEZA ZERO.ilikuhakikisha wanafunzi katika mkoa wa Mara wanafunzi wanendelea kufanya vizuri.

‘Nimeanza na hili hapa katika manispaa ya Musoma na lengo langu zaidi nikuhakikisha nashirikiana na wadau kutatua changamoto za kielimu kuondoa tatizo la zero kwa mkoa wetu tunahitaji kurudi kama zamani katuika kufanya vyema katika matokeo ya kitaifa’Alisem Agness Marwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara.

Aksihiriki katika zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka alisema kampeni ya kutokomeza zero itaenda sambamba katika mapambano dhidi ya Utoro kwa wanafunzi wote kuhakikisha tunachukua hatua kali kwa wale watotoi ambao wamekuwa wakihudhuria shule kwa kusuasua.

Pia chikoka amewataka watendaji kwenda kusimamia swala la chakula kikamilifu mashuleni na swla hilo nilalazimiza sila hiali katika mkoa wa wilaya ya Musoma.

Baadhi ya walimu waliopata tuzo na zwadi hizo wamesema sasa zinaenda kuwa cahcha ya kuongeza ufaulu lakini pia kuwakumbusha kuongeza nguvu katika mapambano ya kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani.







Powered by Blogger.