MEI MOSI KITAIFA IRINGA ,RAIS JPM KWA MARA YA KWANZA KUTUA IRINGA
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kulia akiwapongeza viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi |
![]() |
| Wajumbe wa TUCTA wakiimba wimbo wa wafanyakazi leo |
![]() |
| Wimbo wa kuwaunganisha wafanyakazi |
Rais wa shirikisho la vyama huru
vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya kulia akiwa na
wajumbe wenzake .
SHIRIKISHO la vyama huru vya
wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao ni waandaaji wa sherehe za
wafanyakazi kitaifa (MEI MOSI) wamempongeza Rais Dkt John Magufuli
kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo
za Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa .
Rais wa shirikisho la vyama huru
vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya alisema leo
kuwa katika sherehe hizo za wafanyakazi duniani kwa Tanzania
zitafanyika katika mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa Samora na
kuwa tayari Rais Dkt Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi .
Hivyo aliwataka wafanyakazi
kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe hizo na kuwa kupitia
sherehe hizo watapata fursa ya kujua mikakati ya serikali dhidi ya
wafanyakazi nchini japo hadi sasa wanapongeza hatua iliyofikiwa
na serikali ya kuwarejesha kazini wafanyakazi waliokuwa
wamesimamishwa kazi kutokana na elimu yao ya darasa la saba.
Rais huyo alisema kuwa TUCTA
imefanya jitihada kubwa za kukutana na serikali kuwapigania
wafanyakazi hao walioondolewa kazini kutokana na elimu yao na
serikali imesikiliza na imewarejesha kazini .
Alisema kuwa serikali imeendelea
kufanya jitihada kubwa kuongeza ajira pamoja na kusikiliza kero
mbali mbali za wafanyakazi na kuzipatia majibu .
Akielezea juu ya maandalizi ya
sherehe za mei mosi mkoani Iringa alisema kwa sehemu kubwa
maandalizi yanakwenda vizuri na wamepata ratibu ya kuzunguka
wilaya zote za mkoa wa Iringa kutoa elimu pamoja na kututana na
wafanyakazi ili kujua changamoto zao.
" TUCTA inapenda kuishukuru
serikali ya mkoa wa Iringa kwa kukubali kupokea maadhimisho haya
ya Mei mosi 2018 TUCTA kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa
Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza pamoja na waziri wa nchi
ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge ,kazi ,vijana , ajira na watu
wenye ulemavu Jenista Mhagama tumefanya maandalizi ya kutosha"
Alisema kabla ya Mei mosi mambo
yakayofanyika Iringa ni pamoja na makongamano mawili ya kimkoa na
moja la kitaifa na kuwakongamano la kwanza litafanyika April 23
katika wilaya ya Mufindi ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya
ya Mufindi Jamhuri Wiliam wakati kongamano la pili litafanyika
wilaya ya Kilolo April 25 na mgeni rasmi ni mkuu wa wilaya ya
Kilolo Asia Abdalah huku April 27 litafanyika kongamano la kitaifa
litakalohusu Tanzania ya uchumi wa viwanda kwenye ukumbi wa
Kichangani ambalo viongozi mbali mbali wa kitaifa watashiriki .
Aidha alisema kutakuwa na michezo
ya Mei mosi ya fani mbali mbali itakayoanza April 16 hadi April 30
katika uwanja wa Samora kuwa kwa ajili ya kuwafanya wafanyabiashara
na wajasilia mali kutumia fursa ya mei mosi Iringa maonyesho ya
bidhaa mbali mbali yatafanyika .




