KIGERA ETUMA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA WA ZAHATI YA KIJIJI. MAPEMA KABLA YA MWEZI UJAO.
Picha ni wananchi na viongozi wa kijiji wakiendelea na shughuli ya ujenzi huo.

Na James Francis, Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha Kigera Etuma, Kata ya Nyakatende kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji hicho wamejipanga kukamilisha ujenzi wa Boma la nyumba ya Mganga, kabla ya mwisho wa mwezi wa tano mwaka 2018.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge aliyefika katika eneo hilo , Diwani wa Kata ya Nyakatende Mhe. Rufumbo alisema kuwa wananchi wamekubali kujenga zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati hiyo kijijini hapo.
Rufumbo aliongeza kuwa wakati ujenzi wa nyumba ya Mganga ukienda kwa kasi, bado upo uhitaji wa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha sakafu ya jengo la zahanati hiyo.
“Kiukweli Wananchi wanajituma kwa bidii ili zahanati hiyo ikamilike na kuanza kutumika ifikapo Desemba 2018”Alisema Rufumbo.
Aidha Mbunge kwa kutambua mchango huo wa wananchi na viongozi wa Kijiji cha Kigera Etuma alipongeza kwa uamuzi na ushirikiano wa ujenzi wa zahanati na vyumba vya madarasa kwa Shule za Msingi kijijini hapo.