ATUMBULIWA KWA KUKIUKA KATIBA .

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia baraza kuu la
uongozi Mkoa wa Morogoro limemvua James Mkude nafasi aliyekuwa akiishika
ya Mwenyekiti wa Manispaa ya Morogoro kutokana na tuhuma za kujihusisha
na matukio yaliyo kinyume na katiba ya chama hicho.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambaye pia
ni Mbunge wa jimbo la Mlimba Bi. Suzani Kiwanga na kusema hatua hiyo
imekuja baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizo wasilishwa ndani ya chama
hicho ingawa ni tuhuma binafsi zinazomkabili mwenyekiti huyo
aliyesimamishwa na kwamba hazihusiani na chama.
Akitoa maadhimio ya wajumbe wa baraza la uongozi la chama hicho mkoa wa
Morogoro waliokutana kujadili muenendo wa mwenyekiti huyo, Bi. Suzani
amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 2006 toleo la
mwaka 2016 kifungu cha saba pamoja na maadili ya uongozi kinatoa mamlaka
kwa baraza hilo kumsimamisha mtu yeyote atakae kiuka maadili ya
kinidhamu ya chama hicho.