Waziri Makamba awasisitizia wakazi wa Songwe kutunza vyanzo vya maji
Wakazi
wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji
kwakuwa Maji hayana mbadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye
dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua
mazingira nchini.
Akiwa
katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia
uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya watu,
nahaikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba
amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha
wanambaini watu hao na kuwatisha ka$ka vyombo vya Sheria.
Taarifa
iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa
nauvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za
kuwaondoakwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao
wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia
kutumikamamlaka ya Dola. “Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya
Maji nakuwabembeleza watoke,” Makamba alisisitiza.
Waziri
Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka
zilizopo,ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo
waondolewe kwanguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha
ainishwa. Pia WaziriMakamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo
za Mazingira za Vijijina Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi
ya Mazingira Nchini.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata
yaLubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia,
kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo
vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.
Pia
Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha
Matutaama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko.
AidhaWaziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za
ujenzi wa
Kituo
cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri Makamba
anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.