KAMPENI YA KUPIGA VITA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI YA BINTI WA KITAA YAFANYIKA TABATA JIJINI DAR.
Bibi
Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo
yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia
alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto
wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea
kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto wao.
Furahini Michael akiulizwa swali na Bwana Steven Mfuko kuhusu athari za mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo.
Mkazi
wa Tabata kwa Cecy ambapo kampeni ya Binti wa kitaa ilifanyika
Bi.Sheira Mheni akielezea jinsi watoto hususani wa kike wenye umri kati
ya Miaka 12-17 walivyoharibika kutokana na mabadikiko ya Teknolijia
ambapo imewapekea kufahamu mambo ya wakubwa wakiwa watoto na hatimaye
kupata matamanio na kufanya kama walivyo ona katika Mitandao ya kijamii
na Runinga jambo linalowasababishia Mimba za Utotoni
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo
kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo
zimefanywa na Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa
kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa vinavyosaidia kutatua
tatizo hilo.
Mmoja
wa Mabinti ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anatoa ushuhuda wa
kuachishwa shule,na hapa alipo hasomi na kampeni ya Binti wa kitaa
kupitia wadau watafanya jambo kwa Binti huyu
Mwanaharakati Kijana Victoria Mwanziva akijibu swali na kuelezea kwa kina tafsiri ya Jinsia
Mwezeshaji
wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Steven Mfuko akiwahoji baadhi ya Maswali
watoto hawa wenye umri wa miaka 12 kama wanajua maswala mbalimbali
kuhusu wao na kusema kwamba hawafahamu, na kuomba wapewe elimu juu ya
mabadiko yao ya mwili ili kuepuka Mimba za utotoni
Bi.
Mwama Ajabu akielezea namna Simu zilivyoweza kuwaharibu watoto wa kike
na kuongeza kuwa wazazi hawana muda nao ndio mana hizo simu zimawaharibu
sana, na mara nyingi hufanya mawasiliano kisiri mida ya usiku wakati
watu wamelala na kibaya zaidi watoto hao hupendelea zaidi kufatilia
mitandao ambayo sio mizuri, ameshauri wazazi mwenzake kuwa lazima wawe
karibu na mabinti zao.
Baadhi ya wahusika wa Binti Kitaa wakiongea na Bodaboda waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa
Anna akizungumzia Jinsi Binti wa Kitaa inavyofanya kazi
Hii Timu ya Binti wa kitaa Wakimsikiliza Mtoto aliyeachishwa Shule na Mzazi wake
Baadhi ya wahusika wa Binti wa Kitaa wakiwa katika eneo la tukio
Baadhi ya watu wakiwa katika Mdahalo huo
Mhandisi Eliwanjeria James kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania akielezea kwa kina juu ya kampeni ya Binti wa Kitaa
Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa Ambassador Angelo akiendela kutoa Mwongozo
Mwakilishi wa Sunshine Group akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Binti wa Kitaa
Mwakilishi kutoka GW Health World Limited akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Binti wa Kitaa
Bwana Steven Mfuko akitoa Elimu juu ya Mimba za Utotoni na Kuolewa wakiwa chini ya Miaka 18
Watu mbalimbali wakiwa katika kampeni hiyo
Kulia ni Binti akitoa ushuhuda wa yeye kupata mimba wakati akiwa na miaka 16 na kusema hiyo ilisababishwa na familia yake
Aliyemwakilisha
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye
pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na
Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa
madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha Mimba
nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili
kupiga vita swala hilo
Bwana
nidhamu wa Madereva wa Bodaboda kituo cha Cecy Bwana Atupele akieleza
namna elimu ya maswala ya Jinsia ilivyo wasaidia wao kuunga mkono
kupambana na mimba za utotoni ambapo wamejiwekea utaratibu wa adhabu
kali kwa yeyote atakayempa mimba binti mwenye umri wa chini ya miaka 18
Mambinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa
Mwakilishi
wa Sunshine Group Fatuma akielezea namna mimba za utotoni zinavyo
athiri maisha ya Binti na pia kusababisha matatizo ya kiafya na
kumsababisha akose mambo mengi na kuahidi kuendelea kushirikiana na
kampeni ya Binti wa Kitaa kupinga swala hilo
Mwakilishi
kutoka TBC FM akielezea majukumu yao ya kuhakikisha kila mtu anapata
habari na taarifa pia elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni pamoja na
ndoa
Bwana
Makundi kuroka Radio France RFI akielezea namna baadhi ya Nchi zenye
machafuko zinavyo wanyanyasa mabinti wadogo wenye chini ya umri wa miaka
18 kwa kuwaoa, kufanya nao ngono pia kuwahusisha katika mashambulizi
mbalimbali, Pia alieleza kuwa vyombo vya Habari vina jukumu kubwa sana
la kuhakikisha jamii inapata taarifa na elimu juu ya kupinga mimba na
ndoa za utotoni
Kila
sehemu ambapo Kampeni ya Binti wa Kitaa inapita huwa panaachwa alama
inayo onesha kuwa kuna kitu kilifanyika hapa Meneja wa Kampeni ya Binti
wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James (kushoto) akiwa na mtoto ambaye
aliachishwa shule na Baba yake , hapa anakabidhiwa rasmi kwa wawakilishi
wa Sunshine Group Ltd pamoja na GW Health limited kwa ajili ya
kusomeshwa ili amalizie masomo yake
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje