TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
TELEGRAMS:
POLISI,
OFISI YA
TELEPHONE: 2500712 KAMANDA
WA POLISI,
Fax:
2502310 MKOA WA MWANZA,
E-mail:
mwapol@yahoo.com S.L.P.
120,
rpc.mwanza@tpf.go.tz MWANZA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA
VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 20.10.2016
· WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKAMATWA WAKIWA NA SILAHA MBILI NA RISASI ISHIRINI NA
TATU WILAYANI ILEMELA WAKITUHUMIWA KUFANYA UHALIFU.
· WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKAMATWA WAKIWA WANATAKA KUUZA GARI WALILOKUWA WAMELIIBA
HUKO JIJINI DAR ES SAALAM.
· MTU MMOJA AMEUAWA KWA KUKATWA NA
VITU VYENYE NCHA KALI NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA WILAYANI MAGU.
KWAMBA
TAREHE 18.10.2016 MAJIRA YA SAA 13:00HRS KATIKA ENEO LA BUSWELU KATA YA BUSWELU
WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KATIKA MISAKO NA DORIA WALIFANIKIWA
KUWAKAMATA WATU SITA WAKIWA NA SILAHA MBILI ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI PAMOJA NA
RISASI ISHIRINI NA TATU, AMBAZO WALIKUWA WAKIZITUMIA KATIKA MATUKIO YA
UNYANG’ANYI WA MALI NA UPORAJI HAPA JIJINI MWANZA NA MIKOA MINGINE.
AIDHA
TUKIO HILO LIMEFANIKIWA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KUHUSU
UWEPO WA WAHALIFU HAO, NDIPO ASKARI WALIFANIKIWA KUMKAMATA KWANZA JEREMIAH
MALIGIA @ MKUMBO MIAKA 25, MNYIRAMBA, FUNDI SEREMALA MKAZI WA MALEGA – SINGIDA
AMBAYE ALIPOHOJIWA ALIKIRI KUHUSIKA NA KUTAJA WENZAKE WALIOKUWA WAKISHIRIKIANA,
NA KUWA SILAHA WAMEZIFICHA KWA MGANGA WA KIENYEJI AITWAYE LEORNAD LITTA @ MAKAI
ANAYEISHI MTAA WA KAGIDA - BUSWELU.
ASKARI
WALIKWENDA MAHALI HAPO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MGANGA HUYO WA KIENYEJI BWANA
LEORNAD LITTA MIAKA 39, AKIWA NA SILAHA
HIZO MBILI ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI HAPO NYUMBANI KWAKE NA RISASI ISHIRINI NA
MBILI ZINAZOTUMIWA NA BUNDUKI YA AINA YA SHORT GUN NA RISASI MOJA YA RIFLE AINA
YA MARK IV.
AIDHA
KATIKA KUHOJIWA ZAIDI NA ASKARI
WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WALIWATAJA WASHIRIKA WAO WANNE AMBAO WALIKUWA
WAKISHIRIKIANA KATIKA KUFANYA UHALIFU AMBAPO ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA,
AMBAO NI 1. KAMGISHA JOVINI KAMHAMBWA MIAKA 40, MLINZI NA MKAZI WA ILOGANZALA,
2. JUMA YUSUPH @ JIMI MIAKA 35, MKAZI WA BWANI KINONDONI, 3. SAMWELI PETER
MIAKA 36, MKAZI WA BUSWELI NA 4. SHABANI HUSSEIN MIAKA 26, FUNDI VIATU NA MKAZI
WA NYASAKA MSUMBIJI.
WATUHUMIWA
WOTE WALIPOFANYIWA MAHOJIANO WALIKIRI KWAMBA SILAHA HIZO WALIZITUMIA KATIKA
UNYANG’ANYI WA MALI NA UPORAJI KATIKA MAENEO YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AIDHA
JESHI LA POLISI KWA SASA LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO NA
MATUKIO WALIYOKUWA WAMEYAFANYA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE
WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA NA TABIA YA KUTOA
USHIRIKIANO KWA JESHI LAO LA POLISI, ILI TUWEZE KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA
WETU., LAKINI PIA ANATOA ANGALIZO KWA WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA
TABIA
YA KUJIHUSISHA NA UHALIFU BALI WAJIKITE KATIKA KUFANYA SHUGHULI HALALI ZA
MAENDELEO, KWANI JESHI LA POLISI LIPO VIZURI
KUHAKIKISHA
ULINZI NA USALAMA UPO KWA RAIA WOTE WA JIJI NA MKOA WA MWANZA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MNAMO
TAREHE 18.10.2016 MAJIRA YA SAA 14:00HRS MCHANA KATIKA ENEO LA ILEMELA WILAYA YA
ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WAWILI
AMBAO NI 1. RAHIM FEKA MIAKA 28, MKAZI WA ILALA – DAR ES SALAAM, 2. ALLY KAWALALE MIAKA 32, MKAZI WA JETRUMO –
ARPORT DAR ES SALAAM, WAKIWA WANATAKA KUUZA GARI LENYE NAMBA T.778 AZV AINA YA
TOYOTA LAND CRUISER LILILOKUWA WAMELIIBA HUKO ILALA JIJINI DAR ES SALAAM.
AIDHA
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA BAADA YA
KUPOKELEWA TAARIFA YA KUIBIWA KWA GARI HILO HUKO DAR ES SALAAM NA KWAMBA KUNA
UWEZEKANO KUWEPO ENEO LA KANDA YA ZIWA, NDIPO ULIFANYIKA UPELELZI KUHUSIANA NA
TAARIFA HIYO, NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WAKIWA NA GARI
HILO.
WATUHUMIWA
WOTE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI WAKIENDELEA NA MAHOJIANO , HUKU
TARATIBU ZA KUWASAFIRISHA KWENDA DAR ES SALAAM WAKIWA CHINI YA ULINZI WA ASKARI POLISI ZIKIWA BADO ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI
WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUNUNUA VITU VYA WIZI, BALI
PINDI WANAPOONA BIASHARA ZA WIZI ZINATAKA KUFANYIKA AU ZINAFANYIKA WATOE
TAARIFA POLISI ILI WATUHUMIWA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA TATU
KWAMBA
TAREHE 18.10.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA IBUNGIRO KIJIJI
CHA SAGANI KATA YA KANDAWE WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MSICHANA ALIYEJULIKANA
KWA JINA LA DEMA CHARLES @ BULAYI MIAKA 20, MKAZI WA KANDAWE, AMEUAWA KWA
KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA KIUNONI
AKIWA
AMELALALA NA WATU WASIOJULIKANA, HUKU WENZAKE WA WILI WAKIJERUHIWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MIILI YAO.
MAJERUHI
WALIOJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO NI 1.MARIAM LUCAS @ KAPELE MIAKA 26, MKAZI
WA KIJIJI CHA SAGANI ALIYEJERUHIWA SHINGONI NA KWENYE KIGANJA CHA MKONO WA
KULIA, 2. KAPELELE MAKUBI @ SALULO MIAKA 90, AMBAYE NI BABA MWENYE NYUMBA/ MJI,
ALIYEJERUHIWA MGONGONI, KICHWANI NA KIUNONI.
INADAIWA
KUWA WAUAJI HAO WALIFIKA KATIKA NYUMBA HIYO MAJIRA TAJWA HAPO JUU NA KUWAKUTA
WENYE MJI WAKIWA WAMELALA, NDIPO
WALIINGIA NDANI NA KUFANYA MAUAJI HAYO, HADI SASA HAKUNA MTU YEYOTE
ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
AIDHA
UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINISHA KUWA MAUJI HAYO YAMETOKANA NA KULIPIZA KISASI,
JESHI LA POLISI KWA SASA LIPO KATIKA UPELEZI PAMOJA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA
TUKIO HILO, MAJERUHI WAPO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU WAKIENDELEA
KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA
POLISI ILI WATUHUMIWA WA MAUAJI HAYO WAWEZWE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA
VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA
NA:
DCP:
AHMED MSANGI
KAMANDA
WA POLISI (M) MWANZA