Utafiti umetaja nchi za Afrika ambazo ni hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli
Taarifa
hii imeripotiwa na BBC ambapo imesema kuwa Shirika la mazingira la
Umoja wa mataifa UNEP limesema kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki
dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, 49% ni watu
wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki
.
Utafiti
wa umoja wa mataifa kuhusu ajali za barabarani umezitaja nchi za
Malawi, Kenya na Afrika kusini kuwa nchi hatari zaidi kutembea kwa miguu
na kuendesha baiskeli,
Takwimu za watu waliokufa wakitembea au wanapoendesha baiskeli katika ajali za barabarani:
- Malawi: 49% wanaotembea, 14-17% wanaoendesha baiskeli
- Kenya: 47% wanaotembea, 14% wanaoendesha baiskeli
- Afrika kusini: 50% wanaotembea, 3% wanaoendesha baiskeli.
UNEP
imesema uwekezaji wa dharura unahitajika kuimarisha miundombinu ya
kutembea na kuendesha baiskeli ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
Ripoti ya
utafiti huo wa UNEP iliyopewa jina ‘Global Outlook on Walking and
Cycling’, inaeleza kuwa ukosefu wa uwekezaji katika kuhakikisha watu
wanatembea na kuendesha baiskeli salama ndiyo unaochangia vifo vya
mamilioni ya watu na kupuuza nafasi nzuri ya kuchangia katika vita dhidi
ya mabadiliko ya hali ya hewa.
SOURCE: BBC