Watu tisa watiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali.
JESHI la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kufanya uhalifu wakiwa na silaha mbili zilizotengenezwa kienyeji zikiwa na risasi 23 ambazo walikuwa wakizitumia katika matukio ya unyang’anyi wa mali na uporaji.
Tukio hilo lililitokea oktomber 18 majira ya saa saba usiku ambapo askari waliwakamata watuhumiwa Jeremia Maligia (25), Leornad Litta (39), Kamgisha Kamhambwa (40), Juma Yusuph (35), Samweli Peter(36) na Shabani Husseni (26) ambapo watuhumiwa walikiri kuzitumia siraha hizo kwa matukio mbalimbali.
Hivyo jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na matukio waliyokuwa wameyafanya pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa mashaksamini.
Aidha watuhumiwa wawili wakazi wa Dar es salaam Rahim Feka(28) na Ally Kawalale (32) nao wanashikiliwa kwa kosa la kutaka kuuza gari lenye namba T.778 AZV aina ya Toyota land cruiser waliloiba huko Ilala Jijini Dar es salam.
Watuhumiwa hao walikamatwa baada jeshi hilo kupokea taarifa kuibiwa kwa gari hilo, ndipo upelelezi ulipofanyika na kufanikiwa kuwakamata katika eneo la Ilemela Jijini hapa wakiwa wanataka kuliuza .
Hivyo mpaka sasa wapo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi wakiendelea na mahojiano ,huku taratibu za kuwasafirisha kwenda Dar es salamu wakiwa chini ya ulinzi wa askari polisi zikiwa bado zinaendelea .
Aidha wakati huohuo mtu moja aliyetambulika kwa jina la Hamed Gambo (22) mkazi wa Kigoma, anashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kukutwa na sale za jeshi hilo mali ya askari namba H6332 Pc Mriha alizoziba msikitini wakati askari huyo akiwa anaendelea na ibaada na kuacha begi nje ambapo mtuhumiwa huyo alizitumia nguo hizo kuwatapeli wananchi.
Vivyo hivyo jeshi hilo bado linaendelea na msako wa wauwaji wa Dema Charlers (20) mkazi wa Ibungiro kijiji cha Sagani wilayani magu aliyeuwawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kiunoni na watu wasiojulikana saa tano usiku akiwa amelala na wenzake wawili ambao walijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili yao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapomtilia mtu mashaka katika vitendo vya uvunjifu wa amani, ili watuhumiwa waweze kukamatwa jambo hilo litasaidia kudhibiti uhalifu .