TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MWANZA
01.10.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA MTAA WA KANYERERE KATA YA BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PAUL JONES @ KINA, MIAKA 34, MZANAKI, MWENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKAZI WA MTAA WA KANYERERE, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KUMZAA JINA LINAHIFADHIWA, MWENYE UMRI WA MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI TAMBUKA RELI, BAADA YA KUPATIKANA KWA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA TAJWA
HAPO JUU ALIKUWA NA KAWAIDA (TABIA) YA KUMBAKA BINTI YAKE KWA MUDA
MREFU, NDIPO WATU WAKARIBU MAJIRANI WALIWEZA KUTOA TAARIFA POLISI
KUHUSIANA NA KITENDO HICHO, AIDHA BINTI ALIWEZA KUPELEKWA HOSPITALI KWA
AJILI YA UCHUNGUZI NDIPO IKATHIBITIKA KWAMBA NI KWELI AMEBAKWA.
MTUHUMIWA WA KITENDO HICHO CHA
UBAKAJI AMEKAMATWA YUPO NDANI, TAYARI JALADA LAKE LA MASHITAKA
LIMEPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI, HIVYO MUDA WOWOTE KUANZIA HIVI
SASA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA
DHIDI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA
MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA WATU WOTE WENYE KESI ZA AINA KAMA HIYO ZA
KUBAKWA AU UNYANYASAJI WA KIJINSIA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI
NA MAHAKAMA, LAKINI PIA ANAWAKUMBUSHA MASHAHIDI WA KESI ZA AINA KAMA
HII KUACHA TABIA YA KUMALIZANA KIENYEJI NYUMBANI HADI KUPELEKEA KESI
NYINGI KUHARIBIKA BALI MASHAHIDI WANATAKIWA WAKATOE USHAHIDI MAHAKAMANI
ILI HAKI IWEZE KUPATIKANA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA