VIONGOZI WA MILA WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO
Viongozi wa Mila wa jamii ya
Wamasai wametakiwa kusuluhisha na kutatua migogoro ya ardhi,maeneo ya
malisho pamoja na wizi wa mifugo ili kuepusha uvunjifu wa amani na
kuzorota kwa maendeleo kunakosababishwa na migogoro hiyo.
Hayo yameelezwa na Wazee wa Mila
Peter Toima na Lemamiye Shininii wakati wa sherehe za kuhama rika
ambao Maelfu wa vijana kutoka Wilaya ya Simanjiro wanahamia rika la
wazee na kukabidhiwa wajibu wa kuwa wasuluhishi katika jamii.
Wazee hao Walisema kuwa jukumu la
kutatua migogoro linapaswa kufanywa na Wazee hao wapya na kuepuka
kuitwisha serikali mzigo mkubwa wa migogoro ambayo wangeweza kuitatua .
Kwa upande wao Vijana waliohama
rika na kuingia rika la wazee Oreka Mlolo na walisema kuwa kazi kubwa
iliyoko mbele yao ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani ,kudumisha
umoja na ushirikiano ambazo ni tunu muhimu kwa jamii ya Wamasai.
Mmoja wa Kinamama ambao Waume zao
wameama rika Loema Thadey alisema kuwa mila hiyo hutumika kupima
uaminifu wa Wanandoa iwapo Mwanamke anachepuka basi anaweza kupoteza
maisha.
Jamii ya Wamasai ni jamii yenye
tamaduni yenye nguvu iliyodumu kwa muda mrefu na kuenziwa licha ya
changamoto ya utandawazi uliomeza tamaduni nyingi za Kiafrika na kuleta
utamaduni wa nchi za Magharibi.