TAARIFA KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE
1.0 UTANGULIZI
Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza tarehe 17 Oktoba hadi
tarehe 30 Oktoba 2016, Mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa
Tano wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 1 Novemba 2016. Kufuatia
Ratiba hiyo ya shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote
wanapaswa kuwa wamewasili Mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 16
Oktoba, 2016 kwa ajili ya kushiriki vikao hivyo.
2.0 SHUGHULI ZILIZOPANGWA KATIKA RATIBA
katika Vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama
ifuatavyo:
- a)KUPOKEAMAONI YA WADAU WA MISWADA MBALIMBALI
Kamati mbili (2) za Kisekta zitajadili Miswada miwili ya Sheria
ambapo Kamati ya Katiba na Sheria itajadili Muswada wa Sheria
ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na. 3 wa Mwaka 2016 [The
Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2016] na itakuwa na
vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya
tarehe 21 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Serengeti, Ofisi ya Hazina
Mjini Dodoma kuanzia saa tano (5:00) Asubuhi ambapo Sheria hiyo
ina jumla ya Sheria 9 zitakazofanyiwa marekebisho na Muswada
huu.
Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
ambayo itajadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa
Mwaka 2016 [The Media Services Bill, 2016] na itakuwa na vikao vya
kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 19
Oktoba, 2016 Katika ukumbi ulipo katika Jengo la Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mjini Dodoma kuanzia saa
tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa(9:000) Alasiri.
Pamoja na kamati hizo mbili za kisekta, pia Kamati ya Sekta
Mtambuka ambayo ni Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo nayo
imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public
Hearing) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali
katika Mkutano wa Nne wa Bunge. Mikutano hiyo inatarajiwa
kufanyika kati ya Jumanne tarehe 18 Oktoba, 2016 na Alhamisi
tarehe 27 Oktoba, 2016 katika Jengo la Hazina (Treasury Square)
Mjini Dodoma.
Wadau wote katika Miswada tajwa hapo juu wanakaribishwa
kufika mbele ya Kamati kutoa maoni yao katika tarehe na muda
uliotajwa.
- b)KUPOKEATAARIFA ZA KIUTENDAJI WA WIZARA
Kamati tisa (9) za kisekta zitapokea Taarifa za utendaji wa Wizara
zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1)
(c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo Januari, 2016.
- i) Kamatiya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama itapokea na
kujadili Taarifa za wawakilishi wa Bunge katika SADC – PF,
ACP – EU na CPA kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (2) (iii) na (iv)
cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016.