Matumizi ya kemikali aina ya Mekyuri yamedaiwa kuhatarisha afya za wananchi Katavi
Matumizi ya kemikali aina ya Mekyuri katika mchakato wa kuchuja dhahabu kwenye machimbo ya madini yaliyoko mkoani Katavi yamedaiwa kuhatarisha afya za wananchi wanaotumia vyakula vinavyopatikana katika bonde la ziwa Rukwa ikiwa ni pamoja na walaji wa samaki wanaovuliwa katika ziwa hilo.
Wadau wa mazingira waliokutana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa wamedaiwa kuwa kemikali hiyo hutiririshwa hadi ziwani hasa nyakati za masika na kuwa sumu kwa binadamu wanaopata mahitaji ya chakula kutoka bonde la ziwa Rukwa.
Hayo yamebainishwa na wadau wa bonde la ziwa Rukwa katika kikao cha kujenga uwezo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa mjini Sumbawanga, Dkt Halfan Haule ni Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga amesisitiza umuhimu wa kuepukana na madhara ya kemikali ya mekyuri inayotumika katika machimbo ya madini.
Katika kutafuta suluhisho la kuepukana na matumizi ya samaki na mazao yanayopatikana katika bonde la ziwa Rukwa shirika la maendeleo la Uholanzi la SNV limewaita pamoja wadau kujadili changamoto mkabala wanaotoka mikoa ya Rukwa, Mbeya, Katavi na Iringa ili kuwa na sauti moja kuzuia matumizi ya kemikali katika migodi ya dhahabu.