MTOTO WA KIKE MWENYE UMRI WA MIEZI 8 ATELEKEZWA NA MAMA YAKE MZAZI
MTOTO
wa kike anayekisiwa kuwa na umri kati ya miezi minane na mwaka mmoja
amefikishwa katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete na wasamaria
wema baada ya kutekelezwa na mama yake mzazi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete , Amina Ali Mabrouk ambaye aliachiwa mtoto huyo na mama yake , alisema mama mzazi wa mtoto huyo alimtelekeza mwanawe siku ya Jumatatu jioni kwa madai anakwenda kutelekeza ibada ya sala ya jioni .
Alieleza
kwamba baada ya kukabidhiwa kichanga hicho , mama mzazi hakutokea tena
ambapo alichukua hatua za kwenda kuripoti kituo cha polisi Wete kwa
hatua za kisheria kwa kuwa mtoto huyo alikuwa anahitaji huduma .
“Nilikuwa
katika biashara zangu kigengeni , mara alitoa mama mmoja hanijui wala
na mimi simjui , alinitaka nimsaidie mtoto ili aende kutekeleza ibada ya
sala lakini kuanzia muda huo sikumuona tena ”alieleza.
Aidha
aliongeza kwamba “Ilipofika saa nne usiku ilinibidi niende kutoa
taarifa kwa sheha na baadaye Polisi ambapo nilitakiwa nimfike leo (jana)
asubuhi , nimefika mapema nikaambiwa nije ofisi ya Ustawi wa jamii ”aliongeza.
Afisa
Ustawi wa Jamii Wilaya hiyo Salma Suleiman amekiri kupokea kichanga
hicho na kusema hatua ya kwanza ni kumpeleka hospitali kwa ajili ya
uchunguzi wa afya yake huku hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa .
Alisema
katika kuhakikisha mama mzazi anapatikana , Ofisi ya ustawi wa jamii
imeanza kuwasiliana na viongozi wa shehia ili kusaidia kupatikana mama
yake ambapo kwa sasa ataendelea kuhifadhiwa na Ofisi ya Ustawi wa jamii.
“Jambo
la kwanza ambalo Ofisi ya Ustawi itafanya ni kumpeleka Hospitali
kufanyiwa uchunguzi w afya mtoto huyo , halafu masuala mengine ya
kumtafuta mama mzazi zitafuatia baadaye ”alieleza.
Baadhi
ya wanawake waliozungumza na mwandishi wa habari hizi , wameitaka
Serikali kumtafuta mama aliyefanya kitendo hicho cha kinyama ili aweze
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Bishara
Mbarawa Mkaazi wa Bopwe Wilayani hapa amesahauri kufanyika uchunguzi wa
kina sababu ambazo zimesababisha kichanga hicho kutekelezwa kwani
huenda ni ugomvi wa kifamilia au ugumu wa maisha.
Alisema iwapo Serikali itafanya uchunguzi na kubaini ni sababu ya ugumu wa maisha , basi ni vyema wakaingizwa kwenye mpango wa TASAF wa kaya maskini ili aweze kukabiliana na hali hiyo na hivyo kuweza kutunza familia yake .
“Serikali
inatakiwa kufanya uchunguzi wa kina ikiwa itabaini sababu ni ukali wa
maisha basi aingizwe kwenye mpango wa TASAF wa kusaidia kaya maskini ili
aweze kulea familia yake , la kama sababu ni nyingine pia Serikali
iangalie jinsi ya kumsaidia ”alisisitiza.
Tukio
hilo limekuwa wakati jamii ikiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa
kike na tiko la kwanza kuripotiwa katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii
katika kipindi cha mwaka huu .