Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla azindua mkakati wa Taifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dodoma


whatsapp-image-2016-10-19-at-13-10-32-1
FATILIA HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE.DR HAMISI KIGWANGALLA.,


Hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla


Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo.  Pia, ninayo furaha kubwa kusimama mbele yenu kama mgeni rasmi katika kuzindua mkakati huu muhimu wa pili wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Pamoja na rasilimali chache tulizonazo, Tanzania imepiga hatua kidogo katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana duniani na haswa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwemo. Utafiti uliofanyika na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani na Taasisi ya NIMR, ya viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza imeonyesha kuongezeka kwa viashiria hivyo.
Idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9%, wanaokunywa pombe ni asilimia 29.3%, wenye uzito uliopita kiasi 34.7%, shinikizo la damu ni asilimia 25.9% na wagonjwa wa kisukari ni asilimia 9.1%. Hii haikubaliki, na ni lazima tuongeze bidii katika kuyashughulikia.
Mkakati huu umekuja wakati muafaka, wakati tunatakiwa kutekeleza Mpango wa Malengo endelevu (Sustainable Development Goals) ambayo kati ya malengo kumi na saba, matatu yanazungumzia jinsi ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, baadhi ya malengo haya ni;
  • Kufikia mwaka 2030, kupunguza moja ya tatu ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili;
  • Kuboresha huduma za kinga na tiba ya utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe;
  • Kufikia mwaka 2020, kupunguza nusu ya idadi ya vifo duniani na ajali za barabarani.
Napenda kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Chama cha kupambana na ugonjwa wa kisukari duniani (World Diabetes Foundation) na chama cha kisukari cha Tanzania (Tanzania Diabetes Association), kwa kuwezesha kupitiwa kwa mkakati wa zamani wa mwaka 2008-2015, na kutengenezwa huu wa sasa, ambao ni wa 2016-2020.
Kwa kushirikiana na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, TDA imeweza kutekeleza mpango wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchi nzima.
Aidha nawashukuru kwa dhati wadau wetu wa Maendeleo kwa misaada mbalimbali ambayo imechangia katika kuboresha Afya za Watanzania.
Ninayo taarifa kuwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya mmeombwa kuteua mtu mmoja atakayeratibu shughuli zote za magonjwa yasiyo ya kuambukiza mikoani na wilayani kwenu. Ni matarajio yangu kuwa mtafanya kazi kwa nguvu na kwa ukaribu zaidi na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza cha Wizara ili huduma hizi ziwafikie watu wote hadi ngazi ya jamii.
Baada ya kusema haya machache , sasa natamka kuwa Mkakati huu wa pili wa kitaifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza umezinduliwa rasmi.
whatsapp-image-2016-10-19-at-13-10-40Dkt.Kigwangwalla akionesha moja ya kitabu hicho kilizhozinduliwa leo na kugawiwa kwa waganga wakuu wote nchini,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt.Zainabu Chaula,kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kambi
whatsapp-image-2016-10-19-at-13-10-37Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla akiwahutubia waganga wakuu wa mikoa na wilaya wakati wa uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwenye mkutano wa mwaka wa wakuu hao unaoendelea mjini Dodoma
whatsapp-image-2016-10-19-at-13-10-43Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi mkakati wa Taifa wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kamb
Powered by Blogger.