MAADHIMISHO YA SIKU YA SACCOS DUNIANI 2016 YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.
MUSSAMAKALI.BLOGSPOT
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani, Stellah Mtayabarwa (kushoto), akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), alipotembelea banda la Saccos la Mamlaka ya Bandari (PTA), katika ufunguzi wa maadhimisho hayo uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani, Stellah Mtayabarwa (kushoto), akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), alipotembelea banda la Saccos la Mamlaka ya Bandari (PTA), katika ufunguzi wa maadhimisho hayo uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya
Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard Kalinga (katikati), akihutubia
wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo, Stellah Mtayabarwa.
Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Habibu
Mhezi (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwakilishi wa
Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mrakibu wa Polisi (SP),
Scholastica Luhamba.
Mjasiriamali Zamda Sasillo (kushoto),
akiwa na wateja walitembelea banda lake katika maadhimisho hayo. Kutoka
kulia ni Magdalena Samkumbi, Lubanzo Kalufya na Ashura Shoka.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na Ofisa Uendeshaji Mkuu, Mfuko wa Pembejeo, Pili Mogasa.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Ofisa Masoko wa Benki ya Posta
Tanzania, Ezekiel Fumbo (kushoto), akimuelekeza Dk. Turuka kazi
mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Viongozi Meza kuu wakipiga makofi wakati wakipokea maandamano ya maadhimisho hayo.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens
Turuka wakati wa ufunguzi wa Siku ya Saccos duniani uliofanyika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
"Vyama vya
akiba na mikopo ni wadau wakubwa wa serikali kwani vinasaidia sana
katika kiinua uchumi wa nchi hivyo hatuna budi kuendelea kushirikiana"
alisema Dk.Turuka.
Dk. Turuka
aliwataka viongozi wa vyama hivyo kumaliza changamoto zao wao wenyewe na
wanachama wao pale zinapotokea badala ya kukimbilia serikalini.
Mwenyekiti wa
Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard
Kalinga alisema vyama hivyo vimepata mafanikio makubwa kwani
wamefanikiwa kuanzisha Saccos 4,000 ambazo zipo hadi vijijini na kuwa na
wanachama milioni 1.5 nchini.
"Sheria namba
sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 imeanza kutumika baada ya
kupata idhini ya Rais mwezi Oktoba 2013 lakini ni dhahiri kuwa kumekuwa
na malalamiko mengi juu ya baadhi ya maeneo yaliyoko kwenye sheria hiyo"
alisema Kalinga.
Alisema licha
ya kupata mafanikio hayo changamoto kubwa waliyonayo ni ushirikishwaji
wa kuandaa sheria inayoongoza vyama vya ushirika nchini.