WAKILI TUNDU LISU AONDOA PINGAMIZI MAHAKAMANI KWENYE KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA BUNDA MJINI.
PICTURE KWA HISANI YA BMG BLOG
Wakili
wa wajibu maombi wa kesi namba moja ya mwaka 2015 ya uchaguzi wa Jimbo
la Bunda Mjini, Tundu Lisu, jana aliomba Mahakama kuu Tanzania
inayoendelea Musoma mkoani Mara, kufutilia mbali shauri hilo kwa madai
ya ushahidi uliotolewa na upande wa waleta maombi hauna uhalali wa
kumuwezesha mteja wake ambaye ni mjibu maombi namba moja Estar Bulaya
kuweza kujitetea.
Hali
hiyo ilijitokeza juzi kufuatia shahidi namba tatu Steven Wasira
kukamilisha ushahidi na mawakili wake ambao ni Cosntantini Mtalemwa,
Ajira Mungula na Yassini Membar, kuileza mahakama kuwa wamekamilisha
ushahidi wao, huku lisu akieleza mahakama kuwa hatoleta shaidi kufuatia
mteja wake kuonekana hana kesi ya kujibu.
Hata
vivyo jana Lisu aliishangaza mahakama hiyo kwa kubadilisha uwamuzi wake
na kuiomba mahakama kesi hiyo ilendelee kusikilizwa,huku akidai
kutoendelea na shauli hakutoipotzea mahakama muda,ikiwa leo atamleta
shahidi namba moja kuja kutoa ushahidi ambaye ni mbunge wa jimbo la
Bunda Mjini Estar Bulaya.
“Jana
(juzi) niliiomba Mahakam kufutilia mbali shauri hili kufuatia ushahidi
ulioletwa na upande wa waleta maombi haujajitosheleza kudhibitisha
tuhuma zilizopo katika hati ya maombi kwa kiwango kinachotakiwa, hivyo
tuliiomba Mahakama itoe ruhusa ya kutokuwepo hoja ya wajibu maombi
kujitetea,lakini tumekaa tukatafakari na kushauriana tukaona tuliondoe
pingamizi hilo, hivyo kutokana na kutokamika kwa ushahidi huo
hatutoacha kujibu tuhuma hizo naiomba mahakama iendelee na shauri
hilo,nashadi leo ataoa ushahidi ni Estar Bulaya ,”alisema Lisu.
Aidha
kwa Upande wa waleta maombi wakili Ajira Mungula aliiomba mahakama
kutopokea vielezo ambayo havikuwepo tokea vilipotakiwa kupelekwa mnamo
Desemba 28 mwaka jana wakati vielelezo vyote vilitakiwa kuwasilishwa
kesi ilipoanza kusajiliwa na ni mwaka sasa umepita hadi kufikia hiyo
jana, kufuatia Mwanasheria mkuu wa serikali Angela Lushagabala kuiomba
makama ikubalinenaye kupokea vielezo vya mjibu maombi namba mbili na
tatu pindi atakapo viwakilisha mahali hapo.
Aidha
Jaji Noel Chocha baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili alisema,
mahakama imeridhia hoja ya Lisu yakutokuwepo na hoja ya kujibu
mahakamani hivyo mahakama ilmekubaliana naye kuliondoa pingamizi
lake,huku akitoa maelekezo ya utetezi wa mjibu maombi Esta Bulaya
utaanza leo na mjibu maombi namba mbili na namba tatu utafuata mara
baada ya mjibu maombi wa kwanza kumaliza.
Chocha
alisema maamuzi ya maombi ya kuleta vielelezo vitajibiwa leo Asubuhi
kabla ya kuanza kusikiliza shauri,huku akiahilisha kesi hiyo hadi 0ctoba
12 Mwaka huu.