MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI, BARAZA LA WOTOTO MKOANI MWANZA LATAKA MTOTO WA KIKE KUPEWA FURSA SAWA KATIKA JAMII.
Mwenyekiti wa Baraza
la Watoto mkoani Mwanza, Paulina Mashauri, akizungumza wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza
yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na
kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza la Watoto mkoani Mwanza, akizungumza
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini
Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na
kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Mwanafunzi James John
kutoka shule ya msingi Kitangiri A Jijini Mwanza akizumzia Maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii
leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha ambapo
amesema haungi mkono baadhi ya vitendo wanavyofanyiwa watoto wa kike
ikiwemo unyanyasaji kama vile ubakaji, mimba na ndoa za utotoni.
Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, akizungumza kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii
leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto
kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Mmoja wa vijana walioshiriki kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii
leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto
kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali
Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali
Kulikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo wanafunzi kuonesha uwezo wao wa kujibu maswali
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akitoa ufafanuzi wa jambo
Baraza la
Watoto mkoani Mwanza limeitaka jamii kutoa fursa sawa ya malezi bora kwa watoto
wa kike kama ilivyo kwa watoto wa kiume katika masuala mbalimbali ikiwemo fursa
ya kupata elimu.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Paulina Mashauri, ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike
Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika katika Uwanja wa Furahisha na
kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Naye Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza hilo amesema
bado watoto wa kike wanakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa fursa
ya kupata elimu, mimba na ndoa za utotoni hivyo ni vyema
jamii ikaungana pamoja katika kutokomeza changamoto hizo.
Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, ameiomba
jamii na serikali kwa ujumla kutoa kipaumbele kwa watoto wa kike katika masuala
mbalimbali ikiwemo ya kupata elimu pamoja na fursa za kiuongozi.
PICHA KWA HISANI YA BMG