BABA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAYE WA MIAKA 10 JIJINI MWANZA.
Wakati leo
dunia inaadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike, bado watoto wa kike
wanakabiriwa na changamoto zile zile za miaka mingi ikiwemo ubakaji,
mimba za utoto, ndoa za utotoni na kukosa fursa ya kusoma ikilinganishwa
na watoto wa kiume.
Jijini Mwanza
baba mmoja anayejulikana na kwa jina la Paul Jonas (34) mkazi wa mtaa
Kanyerere, Kata ya Butimba Jijini Mwanza, anashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa kumzaa (10) jina linahifadhiwa,
kwa zaidi ya miaka miwili.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Mwandamizi wa polisi, Ahamed Msangi,
amesema jalada la tuhuma hizo tayari limepelekwa kwa mwanasheria wa
serikali, hivyo muda wowote kuanzia hivi sasa atafikishwa mahakamani,
ili hatua za kisheria ziweze kufuatwa juu ya tukio hilo.
Inasemekana
kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu alikuwa na kawaida (tabia) ya kumbaka
binti yake kwa muda mrefu, kabla ya ndugu kumfumania na kutoa taarifa
kwa uongozi wa kijiji na taarifa polisi kuhusiana na kitendo hicho.
Msangi alieleza
kuwa baadae binti aliweza kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi
ndipo ikathibitika kwamba ni kweli amebakwa.
Kwa mjibu wa
mtoto aliyekuwa akitendewa kitendo hich alisema kuwa toka baba yake
mzazi alipotengana na mama yake mzazi amekuwa akimfanyia kiitendo hicho
kwa kumlaza kila alipokuwa akitegeshea watu wote hawapo nyumbani hapo.
Alieleza kuwa
kutokana na kitendo hicho kutomfurahisha aliwahi kumwambia bibi yake ile
anachofanyiwa lakiniu bibi yake alikataa kumwamini kabla ya ndugu ambao
ni kaka zake kumkuta baba huyo akimbaka na kuwa chanzo cha kugundulika
uovu huo.
“Mimi naomba
mahakama imhukumu kifungo cha maisha maana kitendo alichokifanya ni
kibaya kwenye maisha yangu ya badae na zaidi nilisikia akiapa kumuua
bibi yangu pindi hatakapo toka kifungoni”, alieleza mtoto huyo kwa
masikitiko makubwa.
Kwa upande wake
Erick Karongo afisa uelimishaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la
foundation Karibu Tanzania (FKT) ambalo linajishughulisha na kupinga
ukatili wa kijinsia limeaasa wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao
ili kuwakinga na ukatili ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara.