RC MARA AZINDUA KAMPENI YA CHANJO YA POLIO AWAMU YA TATU MARA








Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evance Mtambi leo agosti 27 2026 amezindua chanjo ya polio awamu ya tatu kwenye wilaya ya Butiama,shule ya msingi Butiama B.


Kwenye uzinduzi huo RC Mtambi ametoa pongezi kwa juhudi zilizofanyika kufanikisha awamu ya kwanza na ya pili ya chanjo hiyo ambayo imezid malengo yaliyoweka ambayo yaliyokua kufikia watoto laki nane na kwenda milioni moja.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Mara kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo ili kuwakinga na ugonjwa huo wenye athari kama kuleta ulemavu kwa watototo.

Kwa Upande wake Daktari Joseph Mdachi kutoka wizara ya Afya nae ameupa pongezi mkoa wa Mara kwa kufanya vyema kwenye awamu mbili zilizopita na ametoa rai kufanya vizuri kwa awamu hii ya ratu ili kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa wa polio.

Katika hatua nyingine Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mara Bi Flowina Muuzaje amesema maandalizi ya utoaji wa chanjo yamekamilika. Watoa huduma wapo tayari kwa chanjo, vitendea kazi vipo na mategemo nikufikia takribani watoto 1,048727 au zaidi kutokanana na walivojipanga.


Powered by Blogger.