MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MARA GHATI CHOMETE KUWAKATIA WATU 120 BIMA ZA AFYA.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Ghati Chomete
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Ghati Chomete ameahidi kuwakatia Bima ya Afya watu 120 ikiwa nimkakati wa kuunga mkono maono na njozi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kila mwananchi kuwa na bima ya Afya.
Chomete alitoa kauli hiyo katika kongamano maalum aliloliandaa a,balo limefanyika katika ukumbi wa CMG wilayani Tarime mkoani Mara ambapo amesema amewiwa kufanya hivyo ilikuzisaidia kaya ambazo hazinauwezo wa kumudu gharama hiyo.
“Nimewiwa katika kongamano hilo kutengeneza Tabasamu kwa watu 120 kuwakati bima za afya ilikuhakikisha wanakuwa na furaha na wenye Afya njema”Alisema Ghati Chomete Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mara