TRA MARA YAGAWA BIDHAA ZILIZOKAMATWA KWANJIA YA MAGENDO
Na Mussa
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Mara imegawa bidhaa mbalimbali katika Taasisi za serikali ikiwemo magereza zilizokamatwa baada ya kuingizwa nchini kwanjia zisizo rasmi (MAGENDO)katika eneo la sirari wilayani Tarime mkoani Mara .
Akizungumza baada ya kumaliza kutekeleza zoezi hilo la ugawaji Meneja wa TRA mkoa wa Mara Masawa masatu amesema wamegawa bidhaa hizo zilizokamatwa baada ya kuingizwa nchini bila kufata taratibu za kiforodha katika eneo la sirari.
Amesema kama wananchi wataingiza bidhaa zao pasipokufata taratibu kuna hatari wengi wao kupoteza mitaji huku akiwataka kuitumia mamlaka ya mapato kupata uelewa juu ya ungizaji wa bidhaa hizo kwani mamlaka imekuwa ikitoa ushirikiano nakuwasaidia wafanya biashara.
“Tumekuwa tukiendelea na misako ilikuhakikisha bidhaa zinazoingia zinafata utaratibu ilikuhakikisha tunawalinda watumiaji na walaji nasisi tutaendelea kutoa elimu kupitia kitengo chetu cha Elimu”Alisema Masawa Masatu Meneja wa TRA mkoa wa Mara.
Kwa upande wake meneja msaidizi mkoa wa Mara Abdallah Mambi amesema bidhaa zilizokamatwa katika oparesheni hiyo nipamoja na Saruji ,Magogo,mchele na sukari na mbolea ndio bidhaa zilizokamatwa katika eneo hilo.
Baadhi ya wakuu wa Taasisi zilizonufaika na mgao wa bidhaa hizo ikiwemo Magereza nahapa mkuu wa Gereza wilayani Tarime mkoani Mara mrakibu wa magereza Sebastian Dioniz amekiri kupokea bidhaa mbalimbali huku akiwataka wananchi kuendelea kufata sheria katika maeneo ya badala ya kufanya biashara kwa kukwepa kodi kwani nihatari katika mitaji yao.
Aidha Bidhaa hizo zimepelekwa katika tassi mbalimbali za serikali ikiwemo magereza na halmshauri ya wilaya Tarime ambayo imepokea mifuko ya mbolea huku mkuu wa gereza wilaya ya Tarime Sebastian Dionis akimuomba meneja wa TRA Mkoa wa Mara kuwakumbuka katika sukari ikiwezekana na chakula kwani ndio hitaji kwao mhimu.