SERIKALI YATOA SHILINGI BIL. 1 KUKATABATI BWAWA LA NYANGOKOLWA.

 





MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew, amesema kuwa Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bil. 1. kwa ajili ya Ukarabati Bwawa la maji,  Nyangokolwa ambalo lilikuwa tegemeo kwa wananchi hao kwa matumizi ya binadamu na Mifugo.

‎Akizunguma leo kwenye Mkutano wa Hadhara, uliofanyika kata ya Nyangokolwa, Mbunge huyo amesema kuwa amesema kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto za wananchi ikiwemo suala la upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama.

‎Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, amekabidhi pampu 18 za maji ambazo zitafungwa kwenye visima ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama.

‎"Tumekuja kutatua changamoto na matatizo ya wananchi, tuweka uwazi, bayana Utekelezaji wa mipango ya serikali, tunataka kujua Mbunge wenu amewateteaje akiwa Bungeni...tumekuja kushukuru kwa kutupa kazi" amesema na kuongeza.

‎"Tutajenga Shule ya Sekondari hapa, ili kuhakikisha tunaenda zaidi Kwa wananchi wetu, na nimekuja na pampu za maji 18 sababu tumeanza safari ya kutekeleza ahadi hatua kwa hatua ili kufikia 2030 changamoto zote ziwe zimekamilika"

‎Katika hatua nyongine, Mbunge huyo kupitia mkutano wa hadhara, amekabidhi mabati 110 kwa ajili ya kuezekea Vyumba viwili vya madarasa shule mpya ya Msingi Ilalambuli pamoja na Gamondo B mabati 110 kwa ajili ya kuezeka Vyumba viwili vya madarasa.


‎Adha, Mhandisi Kundo pia anekabidhi jumla ya Mifuko ya saruji 200 kwa ajili ya Matale Shule ya Msingi ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa.

MWISHO

Powered by Blogger.