GRUMETI FUND WASHEREHEKEA SIKU YA TWIGA DUNIANI.



Watanzania wametakiwa kuendelea kumlinda na kumthamini twiga, ambaye ni nembo ya Taifa la Tanzania, kwa kutambua mchango wake katika kutangaza utalii, kuhifadhi urithi wa asili na kuwajengea watoto na vijana uelewa  kuhusu umuhimu  wa Twiga  na kudumisha utambulisho wa Taifa .

Kila ifikapo juni 21 dunia huadhimisha siku ya Twiga na kwa Tanzania Mnyama huyu hutumika kama nembo ya Taifa wadau wa uhifadhi Grumeti Fund kupitia idara ya Utafiti na Ubunifu wameanzisha program ya elimu ya Uhifadhi kwa wanafunzi wa shule za msingi ikiwa juhudi za kuendeleza uhifadhi wa wamnyama huyo kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa idara Utafiti na Ubunifu Grumeti Fund Dk.George Lohay alisema wameanza kujenga elimu hiyo kwa watoto ilikuwasaidia kuutambua uhifadhi kwa watoto wakiwa wadogo nahiyo nikutimiza lengo la kuwarithisha.

“Tunamsherehekea Mnyama Twiga ninembo Taifa nimnyama Mpole ambae pia anapendwa sana na watalii kwahiyo watoto walioko katika hifadhi tunajitahidi sana kuwafundisha watoto”Alisema Dkt George Lohay Mkuu wa Idara Rise Grumeti Fund.

Kwa uapnde wake mkuu kitengo cha maliasili na ufadhi wa mazingira wilaya ya Bunda Marwa Kitende alisema asilimia kubwa wilaya ya Serengeti inazungukwa na mapori mengi hivyo kuwafundisha watoto itasaidia kuwapa ulewa watoto waweze kuulewa Uhifadhi.

Aidha naye Afisa uhusiano Ujirani mwema Ikorongo na Grumeti Shija Alex amesema kwa sasa mahusino ya imarika kutoka katika kijiji vinavyoishi katika Mapori hayo ya ikorongo na Grumeti wamekuwa na ulewa mzuri dhidi ya Uhifadhi kutokana na elimu inayotolewa mara kwa mara huku wananchi wakiomba matamasha hayo kuendelea mara kwa mara ilikuendelea kujenga Elimu ya ulelewa kwa wananchi.

Powered by Blogger.