BARRICK NORTH MARA INAVYOWEKA URITHI KWA MTOTO WA AFRICA.

 




Wakati Afrika inatumia mwezi Juni kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kiafrika, fursa inayoipatia jamii wasaa wa kutafakari haki, utu, na mustakabali wa watoto wa Afrika, Kampuni ya Barrick North Mara kupitia Mgodi wa Dhahabu wa imeonesha  njia ya namna ya kuandaa mustakabali mwema wa mtoto wa Afrika, kwa kuhakikisha kwamba urithi pekee na wa uhakika kwake, elimu, inapatikana katika mazingira bora.

Ili kufanikisha hilo tangu mwaka 2019, Barrick imeelekeza shilingi bilioni 26.9 katika miradi 255 ya maendeleo ya jamii kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo,Kati ya kiasi hicho asilimia 35 sawa na shilingi bilioni 9.4 imeelekezwa moja kwa moja katika elimu.

Katika eneo ambalo utoro ulikuwa ni sehemu ya kawaida ya maisha ya watoto, viwango vya kuacha shule vilikuwa juu, na zaidi sana wasichana wanakabiliwa na mazingira magumu zaidi katika safari yao ya elimu, waalimu wanapambana na changamoto ya makazi uwekezaji huo wa Mgodi wa North Mara umekuwa ni mwali angavu wa matumaini katikati ya kiza totoro.

"Kipimo cha kweli cha mafanikio yetu hakiko katika dhahabu tunayochimba, bali katika mustakabali tunaoujenga, kwa watoto hawa ambao ndio uhai wa taifa," Alisema  Juma Kengoe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Genkuru ambaye Kijiji chake ni miongoni mwa vinavyopokea mrabaha wa asilimia 1 kutoka mgodi huo.

Kwa mwaka 2025 Barrick ilikamilisha miradi 25 katika shule za msingi na 26 katika shule za sekondari katika jamii zinazozunguka mgodi ambayo ilihusisha ujenzi wa madarasa ya kisasa yanayochukua nafasi ya miundo chakavu na michache iliyosababisha watoto kusongamana madarasani na ujenzi wa hostel mbili unaoendelea kwa ajili ya watoto wa kike. 


Miradi hiyo pia ilihusisha ujenzi wa nyumba za walimu, kuhakikisha kwamba waalimu wanakuwa katika mazingira bora ya kuishi ili kuwaweka katika nafasi nzuri ya kufundisha vijana na kuwapatia elimu yenye kiwango cha ubora unaostahiki.


 Aidha miradi hiyo ilihusisha kutengeneza madawati, viti na meza kwa ajili ya waalimu na vifaa vya Tehama pamoja na miundombinu ya maji

Mwalimu John Mwita, ambaye amehudumu katika Wilaya ya Tarime kwa zaidi ya miaka 15, anakumbuka changamoto walizopitia.

 "Kulikuwa na nyakati tulifundisha chini ya miti Mvua iliponyesha, masomo yalisimama Leo, tuna kuta, paa, na hata umeme katika baadhi ya madarasa Watoto wetu sasa wanajua maana ya kujifunza kwa heshima," alisema.

Ukiondoa ujenzi wa miundombinu hiyo ya msingi, Barrick imeenda hatua zaidi. 


Kupitia Mpango wa Friends of North Mara, unaofikia shule 10 za sekondari zinazozunguka mgodi, kampuni imekuwa ikitumia matamasha mbali mbali na semina kuyoa elimu inayoziba pengo ambalo hatua nyingine za kielimu hazilizingatii sana, ujuzi wa ziada unaojenga haiba na wasifu wa mtu (soft skills).


Mafunzo hayo ya ziada yanahusisha elimu ya fedha na mafunzo ya uwekezaji, kuwafundisha vijana jinsi ya kuweka akiba, kuwekeza, na kutambua fursa za kiuchumi, kuhakikisha hawatafuti kazi tu bali wanatengeneza kazi, utunzaji wa mazingira ili kuandaa kizazi kinachoelewa usawa kati ya maendeleo na uhifadhi, jambo muhimu katika eneo la uchimbaji madini. Kampeni dhidi ya ukeketaji, ambapo wanajengewa  uwezo wa kuwa na msimamo thabiti dhidi ya ukeketaji, desturi ambayo bado inaendelezwa katika wilaya ya Tarime kwa kiasi kikubwa, kwa kuelimisha wavulana na wasichana pamoja, mpango unashughulikia mizizi ya ukiukwaji huu wa haki za wasichana na pia wanapata elimu ya haki za binadamu, ili kuhakikisha kila mtoto anaelewa utu wake wa asili na haki wanazostahili chini ya sheria za Tanzania na kimataifa.

"Nimetambua kwamba elimu siyo tu kuhusu kufaulu mitihani," anasema Neema Samweli, mnufaika wa mpango wa Friendsof North Mara. "Ni kuhusu kutuandaa vijana kwa maisha, kufanya maamuzi sahihi, kujilinda, na kuchangia kwa maana katika jamii zao."

Kwa Grace Peter, mwenye umri wa miaka 17, mwanafunzi wa kidato cha nne katika moja ya shule zinazoshiriki, mpango umekuwa wa mabadiliko makubwa maishani. 

"Kabla, sikujua chochote kuhusu kuweka akiba au haki zangu kama msichana Sasa nawafundisha dada zangu wadogo kile nilichojifunza nataka kuwa wakili siku moja, kulinda wasichana wengine," Alisema Grace Peter Mnufaika.

Powered by Blogger.