DC SERENGETI AWAONGOZA WAISLAMU KATIKA IFTAR YA NYANSAHO FOUNDATION












Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Angelina Marco amewaongoza waislamu Takribani 1500 wilayani humo kushiriki Iftar iliyoandaliwa na mwasisi wa Nyansaho Foundation ambae pia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa DKT Rhimo Nyansaho huku akiwataka wananchi kuacha Tabia ya kujichukulia Sheria Mkononi.

Angelina ametoa kauli hiyo Wakati akiwaomba waumini wa Dini ya kiisalamu katika iftar hiyo ambapo alisema Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utumike kuwabadilisha wananchi ikiwemo kukoma nakutokujiingiza katika vitendo vya ukatili pamoja na kujichukulia Sheria Mkononi kwenye Maeneo yao.

"Niwaombe Sana wananchi wa Serengeti na waumini wa Dini zote mfungo huu ukatumike kutubadilisha katika matendo yetu hasa wale wanaojichukilia Sheria Mkononi Mambo hayo yasijitokeze Serengeti Kabisa hatutamani kuishi hivyo tupendane"Alisema Angelina Marco Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.


Akizungumza katika hafla hiyo Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Juma Simba Alisema Wilaya ya Serengeti wamejitwisha swala la Ulinzi na Amani Kwan hawako Tayari kuona mtu yeyeyote akijaribu  kuvuruga Kwanza wataanza nae wenyewe kabla hatua zingine hazijachukuliwa atakayebainika kujihusisha na Vitendo visivyo vya kiungwana

Powered by Blogger.