VIKUNDI VYA AKINA MAMA VYAONGOZA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI MUSOMA VIJIJINI.
katikati ni Afisa kilimo wa Kata ya Rusoli Bwana Servas Ngova akiwaelekeza akina mama namna ya kung'olea mashina yaliyoota Zaidi ya Mawili.

Na Verdiana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
Vikundi mbalimbali vikiwemo vya akina mama na vijana wa Jimbo la Musoma Vijijini wameendelea kuwa mstari wa mbele kutekeleza miradi ya kilimo cha Alizeti katika msimu huu wa kilimo.
Kikundi cha Nguvu Kazi kilichopo Kata ya Rusoli Kijijini Buanga ni miongoni mwa vikundi vinavyoendelea kufanya vizuri kutekeleza Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dr. Vincent na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa kulima zao la Alizeti ambapo mpaka sasa wamelima hekari mbili za zao hilo.
Akizungumza Kiongozi wa Kikundi hicho Bi Silaeli alisema , "tumeamua kujikita kwenye kilimo cha mazao ya biashara ambapo kama kikundi tumeanza na hekari mbili za Alizeti" alisema Silaeli.
Hata hivyo, Bi Silaeli amefafanua kuwa, ni msimu wa pili wanalima Alizeti na kupata mafanikio mazuri na sasa wanaendelea kutoa hamasa kwa jamii ili wabadilike haraka kutafuta mafanikio kwa kulima mazao ya biashara.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Rusoli Bwana Servas Ngova ameeleza kuwa, wananchi wa eneo hilo wamehamasika kulima zao hilo baada ya kupewa elimu juu ya kilimo cha Alizeti na Ufuta na faida zake kiuchumi.
Mbegu zimetowa bure na Mbunge wa Jimbo hilo kwa kushirikiana na Halmshuri ya Musoma Vijijini.
Aidha Diwani wa Kata hiyo Mh. Boazi M. Nyeura amesema kumekuwepo na mwamko wa kilimo cha mazao ya biashara (pamba, alizeti na ufuta) kwa wananchi wa Kata yake, jambo ambalo linaleta matumaini mazuri ya kiuchumi ndani ya Kata yake na kwa Jimbo zima la Musoma Vijijini.
Picha hapo chini ni badhi ya Wana-Kikundi wakiwa shambani na Afisa kilimo wa Kata ya Rusoli.
Ofisi ya Mbunge