NFRA YAJIPANGA UZINDUZI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA APRILI 21, 2018
Kaimu
Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi
Vumilia L. Zikankuba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao
cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao
makuu Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018.
Wakuu
wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma
wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichoongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba, Leo 6 Aprili 2018.
Kutoka kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Fredy
Mbonde, Afisa Ugavi NFRA Magreth Salia Kavishe, na Mhandisi Imani
Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA wakifatilia kwa umakini
kikao cha kazi kilichofanyika katika Ofisi za NFRA Mtaa wa Kizota Mjini
Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA na Mratibu wa Mradi wa kuongeza
uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula,
akiwasilisha maelezo mafupi ya namna mradi utakavyotekelezwa wakati wa
kikao kazi cha wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA, Leo 6 Aprili 2018
Kaimu
Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi
Vumilia L. Zikankuba (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye
kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA
Mkao makuu Mjini Dodoma, Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa maendeleo na
Bishara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda (Kshoto), Leo 6 Aprili 2018.
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa (Mb)
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi
kwa mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi
ya chakula katika dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota Mjini
Dodoma.
Hayo
yamebainishwa leo 6 Aprili 2018 na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba wakati
akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na
wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma.
Bi
Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani Milioni
55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni
sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,
amesisitiza kuwa mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9
Disemba 2017 huku akisema Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za
Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje
Sp.o.o) ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA).
Alisema
Mradi utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja
na ukarabati wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo ni
Arusha (Babati), Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga
na Mpanda.
Baada
ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa
250,000 MT zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000 MT)
jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono
Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kupatikana kwa Mradi
huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi
nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha
maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na
mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.
Hifadhi
ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu
ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa
inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.
Pia,
technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa
na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi
chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la
mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.
Katika kikao kazi hicho Kaimu
Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi
Vumilia L. Zikankuba amewasihi wafanyakazi wote wa NFRA kufanya kazi kwa
ushirikiano na kutambua kuwa nidhamu na bidii yao itakuwa chachu ya
mafanikio zaidi katika kuimarisha utendaji wa NFRA.