WAZIRI WA KATIBA NA SHERI ;ZINGATIENI WELEDI KATIKA UANDIKISHAJI WA VYET...



Waziri wa katiba na sheria akizindua mpango wa mpango wa usajili wawatoto
walio na umri chini ya miaka 5 kwa mikoa ya Mara na Simiyu.

Waziri wa katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongea na wakazi wa
Mara na Simiyu katika uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto Walio na

Umri Chini ya Miaka Mitano Mkoa wa Mara na Simiyu ili kupatiwa Vyeti
vya kuzaliwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo Mjini Musoma.


Waziri amewataka wasajili kuhakikisha wanasajili watoto wenye sifa huku
wakiondokana na suala zima la kutumia Mradi huo kwa lengo la
kijinufaisha
Akizindua rasmi mpango huo unaotekelezwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
RITA ambapo Mpaka sasa tayari wamefikia Mikoa 11 ya Tanzania huku Mkoa
wa Mara wakitarajia kusajili watoto 383,285 na Simiyu351,883 walioko
chini ya Miaka Mitano.




Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akionyeshwa Mfumo unatumika katika Usajili huo.



Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akikabidhi mzazi cheti za kuzaliwa kwa ajili ya Mtoto.



Picha ya Pamoja Waziri wa katiba na Sheria pamoja na Wakuu wa Wilaya Mikoa ya Simiyu na Mara



Picha ya Pamoja Waziri wa katiba na Sheria pamoja na Wafanyakazi wa RITA.



Powered by Blogger.