TIMU BIASHARA UNITED MARA YAAANZA MIKAKATI YA KUBORESHA KIKOSI.



UONGOZI wa timu ya Biashara United ya MjiniMusoma mkoani Mara iliyopanda daraja kucheza LigiKuu Tanzania Bara (VPL) msimu ujao, inasaka Shmilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya awali na usajili.


Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Amani Josiah, alisemafedha hizo ni maandalizi ya awali kusajili wachezaji 10watakaoongeza nguvu kwenye kikosi chao ili kuletaushindani kwenye ligi.

Josiah ambaye pia ni Meneja wa Biashara Unitedalisema timu yake inahitaji kuliongezea nguvu benchila ufundi kwa kuongeza watu, ambapo uongozi watimu hiyo umemteua Fulmence Tungaraza kuwaKocha Mkuu wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 (U20).

"Kwa sasa lengo letu ni kusajili wachezaji 10 katikanafasi tofauti kwajili ya msimu ujao wa ligi kuu ili tuwena kikosi kitakacholeta upinzani kwa timu shiriki,kwahiyo tunaendelea kuwaomba wadau wa soka naviongozi mbalimbali wa serikali waendelee kuichangiatimu iingie kambini mapema April, mwaka huu,"alisema.

Josiah mchezaji wa zamani wa Polisi Mara, alisemamikakati yao ni kusajili wachezaji kadhaa na timu hiyo inatarajia kucheza michezo mbali mbali yakirafiki kwajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwaligi kuu. 
chanzo gazeti la Bingwa.
Powered by Blogger.