PROF,MUHONGO AZINDUA MABARAZA YA WAZEE MUSOMA VIJIJINI TIZAMA PICHA NIMEKUWEKEA HAPO.



Sehemu ya Wazee wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huko musoma vijijini.


Prof. Muhongo akizungumza na Baraza la wazee majita.











Jimbo la musoma vijijini limezindua mabaraza ya wazee kwa vijiji 68 ikiwa lengo nikutoa ushawishi , kushauri na kufatilia maswala ya utamaduni, uchumi na maendeleo katika halmashauri ya musoma.
Akizungumza katika uzinduzi wa mabaraza hayo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sopseter Muhongo amesema mabaraza hayo yameundwa kwaajili ya kutoa ushauri kwa uchumi, utamaduni na maendeleo ameongeza kwa kusema kuwa jukumu la mabaraza haya ni kushawishi na ufatiliaji katika swala zima la maendeleo jimboni ikiwa ni pamoja na miumdo mbinu ya elimu, kujenga na kuboresha miundo mbinu ya afya na uhamasishaji wa kilimo cha pamba, alizeti na ufuta bila kuhofia adha ya soko
ufatiliaji wa maendeleo ni wa muhimu sana na kuwasihi kuwa kupitia mabaraza haya wazee wanalojukumu la kusimamia shughuli zote za maendeleo bila kuingilia utawala wa serikari


William Malima mkazi wa chumwi amempongeza Mbunge kwa kuwa na ubunifu kwa kumfananisha na Mwl Nyerere aliye thamini wazee kwa kuchukua maoni na ushauri ulio na hekima na busara kutoka kwao.kupitia mabaraza haya yatasimamia uchumi, utamaduni na maendeleo

Elias Ndaro Diwani kata ya Musanja ameeleza kuwa uzinduzi wa mabaraza ya wazee hawa umekuja wakati muafaka kwani kumekuwepo kwa mgororo wa ardhi katika maeneo ya vijijini hasa msimu huu wa kilimo hivyo kupitia mabaraza haya yataishauri serikari kupima maeneo ili kila mwananchi apate hati miliki yake

Helena Njegere mkazi wa kiriba amesema na wao kama akina mama kupitia mabaraza haya na hekima ya wazee maadili kwa vijana yamerudi kwa upande wa nidhamu, mavazi na utii. Ameongeza kwa kusema kuwa watatoa elimu kwa watoto wa kike kukazania masomo kwani asilimia kubwa ya watoto wa kike shule za sekondari wamekatisha ndoto zao kwa kibeba ujauzito wakiwa shuleni amehaidi kufatilia na kushawishi maendeleo yote kwa ujumla jimboni.
Picha chini ni Mbunge wa Musoma Vijijini akiwa na wazee wa ukanda wa Majita, Bukwaya na Mugango katika uzinduzi wa mabaraza ya wazee

Powered by Blogger.