Makomando 7 wa Marekani wapotea baada ya meli ya kivita kugongwa Japan
![](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/3A7C/production/_96527941_mediaitem96527940.jpg)
Wanajeshi saba wanamaji wa Marekani hawajulikani waliko baada ya meli
yao USS Fitzgerald, kugongana na meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya
Ufilipino, katika pwani ya mashariki mwa Japan.
Walinzi wa pwani ya Japan wametuma maboti tano na ndege mbili katika eneo hilo kusaidia katika shughuli za uokozi.
Msemaji wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako
sehemu za ndani za zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya
manuari hiyo.
Meli ya ACX Crystal ilionekana kugeuka kabla ya jali hiyo kabla ya kuelekea mjini Tokyo
![](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/D3A6/production/_96528145_dddcded5-b01d-49b7-8b2d-29d4ee161034.jpg)
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino ACX Crystal.
Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta
Uharibifu kwenye meli ya mizigo ya ACX
![](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/16F14/production/_96527939_23cad44f-1c61-459d-bbc6-90044ffeb570.jpg)
Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.
Waliojeruhiwa wakiondolewa kutoka meli ya Japan
![](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/121C6/production/_96528147_ea7993c7-5d6e-4523-b463-229dfc022eb6.jpg)
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.
Meli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa
ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan
ya Nagoya na Tokyo.
Yokosuka
![](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/D6B2/production/_96526945_japanyokosuka464160617.png)
Chanzo-BBC