AKAMATWA KWA KUGHUSHI HATI YA KIWANJA.


WAKATI Serikali ya Awamu ya tano, kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikijikita kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na viwanja kwa wananchi mapya yameibuka Simiyu.


Jeshi la Polisi Mkaoni Simiyu limethibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa kughushi hati ya kiiwanja na kuiuza kwa watu wawili.

‘’Ni kweli tumemkamata Genge Ngulimi ambaye amegushi hati ya kiwanja, huku akijipatia fedha kwa njia ya utapeli kwa kuuza hiyo hati hiyo na kupewa shilingi milioni 3.8, taratibu za upepelezi zimekamilika na tumempeleka mahakamani’’ Alisema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu.

Mshongi aliongeza, Mtuhumiwa huyo baada ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, alikimbilia mkoani Geita ambapo baada wasamalia wema kutoa taarifa waliweza kumkamata.

Kufuatia tukio hilo, watu wawili wamejikuta wakikabidhiwa hati ya kiwanja kimoja yenye majina mawili tofauti, huku namba za kiwanja na eneo likionekana ni la aina moja.


Hali hiyo imebainika baada ya aliyekuwa mmiliki halali wa kiwanja hicho Genge Ngulimi kukopa fedha kiasi cha 350,000 kwa Fikiri Seiph huku akiweka dhamana kwa kutumia hati ya kiwanja yenye jina la Emmanuel Kishimba plot no 214 Block E kilichopo eneo la Salunda mjini Bariadi.

Inadaiwa baada ya kukopa fedha hizo akidai ni kwa ajili ya kuuguza ndugu yake, alishindwa kuirejesha kutokana na muda waliokuwa wameahidiana na Fikiri kuisha bila kurejesha fedha hizo.

Baada ya hali hiyo, Genge akiwa na Hati ya kughushi alikubalina na Marco Malima kuuziana kiwanja hichohicho kwa thamani ya shilingi milioni 3,800,000/=.

Marco Malima alisema walifanya makubaliano hayo ya kuuziana kiwanja tarehe 15/1/2018 chenye ukubwa wa mita 30 na upana mita 15 eneo la Salunda.

Aliongeza kuwa waliandikishana kwa Mwenyekiti wa mtaa wa Salunda huku akikabidhiwa hati feki yenye jina la Genge Ngulimi plot no 214 Block E.

Malima aliongeza kuwa baada ya makubaliano hayo alilipa kiasi cha shilingi 350,000/=, na tarehe 17/1/2018 akikamilisha kiasi kilichobakia cha shilingi 300,000/=.

Aliongeza, baada ya muda siku kadhaa, alipigiwa simu na Fikiri ili wakutane na walipokutana walibaini kuwa mmoja kati yao ametapeliwa kwa kupewa hati ya kughushi ambaye ni Malima.

Baada ya Malima kubaini kuwa ametapeli hati hiyo, alitoa taarifa kituo cha polisi wilayani Bariadi na kupewa RB namba BAR/RB/154/2018 kughushi na BR/IR/96/2018.
Baada ya taarifa hiyo kutolewa jeshi la Polisi lilimsaka mtuhumiwa aliyehusika kuuza kiwanja hicho mara mbili na kughushi nyaraka za serikali ambapo walimkamatia mkoani Geita.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Salunda Lazalo Singibala alisema kuwa ni kweli watu hao walifika ofisini kwake kuandikishana kupeana mkopo kwa kudhamini hati ya kiwanja.

Aliongeza kuwa baada siku kadhaa, Genge alimfuata akimtaka kuandikisha kuwa anauza kiwanja kwa Marco ambaye walikabidhina hati ambayo mwenyekiti hakuwa na shaka ya kuikagua huku akidai kuwa baada ya kulipwa fedha atalipa deni kwa Fikiri.

‘’Mimi sikuwa na mashaka na hati hiyo kwa sababu awali kipindi tunaandikishana juu ya mkopo kwa Fikiri, niliikagua na wakati anapokea fedha hizo alidai kuwa hati amechukua kwa Fikiri na baada ya hapo atakamilisha kulipa deni’’ Alisisitiza Singibala.

MWISHO.

Powered by Blogger.