Prf.SOSPETER MUHONGO APANDA MITI KUADHIMISHA SHEREHE ZA UMOJA WAWAZAZI CCM MKOA WA MARA.



Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo alivyoshiriki kupanda miti katika sherehe za jumuiya ya Wazazi Ccm Mkoa wa mara iliyofanyika kijiji cha maneneke.


















Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dr. Vicent Naano alivyoshiriki kukijanaisha musoma vijijini.




















Na Makalinews.
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof, Muhongo ameshiriki katika sherehe za jumuiya ya ummoja wawazazi mkoani mara na kufanikisha zoezi la upandaji miti zaidi ya 2000.
Profesa aliwataka kujitoa wananchi kuhakikisha miti ambayo wanaipanda kuilinda bali wajijengee tabia ya utunzaji wa mazingira wanaoishi.
Ambapo zoezi la kitaifa la upandaji miti likitarajiwa kufanyika rasmi mwezi wa nne hivyo mbunge ameanza mapema kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano ambayo imetoa agizo kwa kila wilaya kupanda miti laki mmoja(100000).

Jimbo la Musoma vijijini mpaka sasa limefanikiwa kupanda jumla ya miti ipatayo zaidi ya 23,000 huku zoezi hilo likiwa niendelevu katika halamsahuri hiyo ya musoma kwa kushirikisha wananchi.

Wakati huo huo,Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Vicent Naano Anney amesema wilaya yake imejipanga vyema kuanda vitalu vya miti ili visambazwe kwa wananchi waanzee kupanda miti hiyo bila malipo yoyote.

Naye katibu wa jumuiya ya wazazi ya ccm mkoa wa mara Bwana Robert Chilamatu alisema kuwa wamejipanga kuanza kilimo cha umawagiliaji huku malengo yao makubwa yakielekezwa kwa zao la alizeti,huku wakitarajia kuanza ufugaji wa kuku wapatao 150.

Katika kuwanga mkono wazazi mbunge wa jimbo hilo Profesa sospeter muhongo ametoa Tani 20 za ulezi ambazo zitapelekwa kati ya kata ya murangi na musanja hivyo kamati itakaa nakupendekeza namna ya kulima zao hilo.

Mkuu wa Wilaya Musoma, aliongeza kuwa watahakikisha wilaya hiyo inakuwa ya ukanda wakijani kutokana na ukame uliopo katika wilaya hiyo kutokana naukataji wa miti hovyo ambapo pia wilaya imejipanga kutoa tozo kwa kila gunia la mkaa Tsh 5000.

Aidha sherehe za wiki ya jumuiya ya umoja wawazazi mkoa wa mara zimefanyika katika kijiji cha maneke kata ya Busambara wilayani musoma mkoani mara.
Powered by Blogger.