WAZIRI MKUU NCHINI TANZANIA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUKAA KWENYE MAENEO YAO YAKAZI HUKO MKOANI MARA.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa akiongea na Wakazi wa Tarime katika Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Serengeti Mjini Tarime
ambapo amesema kuwa Serikali hawatafumbia macho suala zima la Ukatili
wa kijinsia vikiwemo vipigo dhidi ya Mama na Mtoto huku akiwataka wakazi
wa Tarime kubadilika na kuondokana na ukatili huo.
Wananchi wakiwa katika Mkutano wa hadhara viwanja vya Shamba la Bibi Serengeti Mjini Tarime Mkoani
Mara.
Na Makaliblog.MARA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ametoa agizo kwa watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Rorya wanao ishi nje ya halimashauri hiyo kuhamia na kuishi katika halmashauri yao kufuatia watumishi hao kuishi wilaya ya Tarime na maeneo mengine ya jirani.
Majaliwa alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao cha watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo ambapo alisema ifikapo Februari 15 mwaka huu, kila mtumishi ahakikishe amekwisha hamia katika halmashuri yake.
Alisisitiza kuwa wakuu wa idara kufuatilia watumishi hao wanatekeleza agizo hilo ndani ya wakati tajwa huku akisema serikali haitasita kuwachukulia hatua watumishi watakaokaidi agizo lake.
Aliongeza kumekuwapo na tabia ya watumishi kuishi mbali na vituo vyao vya kazi na kupelekea uchelewashaji wa maendeleo pamoja na ufanisi mzuri wa kazi katika vituo vyao.
Waziri mkuu alisema kwa serikali hii ya awamu ya tano inahitaji watumishi wachapa kazi na wenye uwezo katika taaluma zao hivyo watakapohamia katika halshauri hiyo, kazi zitakwenda vizuri na wananchi watapata huduma stahiki na kwa wakati unao takiwa .
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri Charles Chacha alisema agizo hilo la waziri mkuu litatekelezwa ndani ya kipindi husika kwani halmaahauri hiyo ilikuwa katika mchakato wa kuhakikisha watumishi wrote wanaoishi njee ya halmashauri hiyo wanahamia ndani ya halmashauri hiyo.