NABII TITO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTAKA KUJIUA, ANYIMWA DHAMANA
Dodoma.
Mapema siku ya leo Jumatatu Januari 29, 2018, mkazi wa kijiji cha Nong’ona mkoani Dodoma Bwana Tito Machibya maarufu kwa jina la nabii Tito amefikishwa mbele ya hakimu wa wilaya ya Dodoma kujibu tuhuma zinazomkabili.
Nabii Tito anakabiliwa na shtaka la kutaka kujiua alilotenda siku chache tu toka kukamatwa na Jeshi la polisi mkoani hapo kwa tuhuma za kueneza dini inayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Kwa mujibu wa habari iliyoripotiwa na ITV alasiri hii, taarifa kutoka mahakamani zinasema nabii Tito alitaka kujiua kwa kujichana chana na kiwembe sehemu za tumbo ambapo alikutwa na majeraha hayo na dhamana yake imezuiliwa.
source darmpya.com