ARSENAL WAPIGWA TENA 5-1 NYUMBANI, WATOLEWA KWA 10-2
NIMEKUWEKEA NA PICHA ZOTE HAPO CHINI ;
Arsenal
wamezidi kuonyesha udhaifu na kushindilia machungu kwenye mioyo ya
mashabiki wao baada ya kukubali kipigo kingine cha mabao 5-1 na
kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal
wameondolewa na Bayern Munich ambayo iliitwanga Arsenal kwa idadi hiyo
ya 5-1 mjini Munich. Leo imerudia ikiwa ugenini London.
Sasa kikosi cha Arsenal chini ya Arsene Wenger kimeng'olewa kwa jumla ya mabao 10-2.
Arsenal
walitangulia kufunga kupitia Theo Walcott lakini Bayern walisawazisha
kwa mkwaju wa penalti wa Robert Lewandowski, baadaye Arjen Robben,
Douglas Costa na Arturo Vidal akashindilia msumari mara mbili.
Arsenal
starting XI: Ospina, Monreal, Koscielny, Mustafi, Bellerin, Ramsey
(Coquelin), Xhaka, Oxlade-Chamberlain, Giroud (Ozil), Sanchez (Perez),
Walcott
Bayern
Munich starting XI: Neuer, Rafinha, Javi Martinez, Hummels, Alaba,
Vidal, Alonso, Robben (Costa), Thiago (Kimmich), Ribery (Sanches),
Lewandowski